Fahari ya Serengeti

Friday, September 1, 2017

KLABU YA WAPINGA RUSHWA IKORONGO SEC SERENGETI YAKONGA NYOYO ZA WAKIMBIZA MWENGE KITAIFA

 Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Amour Hamad Amour akikabidhi cheti cha ufunguzi wa klabu ya wapinga rushwa Ikorongo sekondari wilayani Serengeti baada ya kuridhishwa na uelewa wa klabu hiyo na kuagiza wafanye midahalo ndani na nje ya shule kuhusiana na athari za rushwa kwa jamii,kiuchumi na kiusalama,mwenge umemaliza mbio zake mkoa wa Mara na kuanza mkoa wa Arusha .
katika wilaya ya Serengeti jumla ya miradi saba imezinduliwa,kuwekwa jiwe la msingi na kufunguliwa ikiwa na thamani ya zaidi ya sh 1.9 bil.
Walinzi wa mwenge wakiwa kwenye majukumu yao
 Katika maswali ya papo kwa na klabu ya wapinga rushwa Ikorongo sekondari ,kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa amekiri kuwa hakuna kama hao kwa uelewa hadi vifungu,na kuwamwagia sifa Takukuru kwa kuwaandaa vema vijana hao ambao watakuwa chachu ya mabadiliko kwa jamii kuepuka kutoa na kupokea rushwa ili kujenga taifa lenye maadili.
 Kila aliyeguswa alijibu sawasawa licha ya kuwa na maswali ya mtego
 Mambo yalivyokuwa Uwanja wa Mbuzi Mugumu

Meza ya klabu ya wapinga rushwa Ikorongo sekondari ikipitiwa na wakimbiza Mwenge kitaifa,hata hivyo mpangilio wao uliwakosha

0 comments:

Post a Comment