Fahari ya Serengeti

Tuesday, November 17, 2015

SAMOTTA WASHUGHULIKIA ENEO KOROFI MJINI MUGUMU SERENGETI

 Mafundi wakiendelea na kazi ili kuhakikisha eneo hilo korofi linadhibitiwa ili kuepusha madhara makubwa ambayo yangeweza kutokea



Monday, November 16, 2015

WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU WAHITIMU CHUO CHA UFUNDI

BAADHI YA WAHITIMU WA MAFUNZO YA UFUNDI WAKIWA UKUMBI WA HALMSHAURI YA WILAYA YA SERENGETI KWA AJILI YA KUPOKEA VIFAA ,HAPA KAZI TU.




DED NAOMI NNKO NA DC ALLY MAFUTAH NDIYO WAKISIKILIZA NASAHA TOKA KWA WAHITIMU KABLA YA KUWAKABIDHI ZAWADI.

HERI MTANISA MRATIBU WA MPANGO AKITOA MAELEZO JINSI ULIVYOTEKELEZWA HADI VIJANA 28 WAKAFUZU MAFUNZO YA UFUNDI CHUO CHA CHIPUKA.
DC AKIKABIDHI VIFAA












WAMAZINGIRA MAGUMU WAHITIMU .
Na SERENGETI MEDIA CENTRE
Novemba19,2015.
Zaidi y ash 34 milioni zimetumika kugharamia masomo ya ufundi na kuwanunulia vifaa vya kazi  vijana  28 wanaoishi katika Mazingira magumu  wilayani Serengeti Mkoa wa Mara kupitia kitengo cha Tacaids.
Mratibu wa Mpango wa kudhibiti Ukimwi halmashauri hiyo Heri Msanisa, amesema hayo wakati wana wakiwakabidhi vijana hao  vifaa kwenye ukumbi wa halmashauri amesema gharama hizo zilijumuisha ada,chakula na malazi ,lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kujitegemea.
.
Mkuu wa wilaya hiyo  Ally Mafutah akikabidhi vifaa kwa vijana hao kutoka kata 28 amesema lengo la serikali kupitia mpango huo ni kuwawezesha kujiajiri kupitia taaluma hiyo,na kuwasisitiza kuunda vikundi vya kazi ili waweze kuendelea kusaidiwa kwa karibu.

Felista Maro mmoja wa wahitimu kutoka kata ya Majimoto amesema utoaji wa masomo hayo bila ubaguzi wa jinsia na kuwa masomo hayo yamewaweza kupata stadi za maisha na kuomba serikali ihakikishe inawekeza zaidi kwenye eneo la kuwajengea uwezo wa ufundi vijana wengi ili kuwawesha kujiajiri
Wanafunzi hao wamefuzu katika masomo ya kozi mbalimbali ikiwemo ufundi magari,useremala,ushonaji na ujenzi,baadhi tayari wameishaanza kazi za kujitolea katika makampuni ya watu binafsi  wilayani hapo.
Mwisho.

KAMPUNI YA SAMOTTA INAYOJENGA BARABARA YA MUGUMU WILAYANI SERENGETI INASUBIRI MAGARI YAPINDUKE NDIPO WASHUGHULIKIE MAENEO WALIYOCHIMBA.

 Hapo ni katikati ya mji wa Mugumu eneo la Kirawira hoteli ,limegeuka kuwa eneo hatarishi chanzo kikiwa ni kampuni inayojenga barabara ya mjini kwa kiwango cha lami kuchimba mitaro kwa muda mrefu na kuiacha bila kuifukia kama inavyoonekana.




 Hatarai harati kubwa eneo hilo kila siku magari yanakwama








 Hata hawa walikwama hapo hapo,



 Hata hii nayo ilikwama hapo hapo,


Saturday, November 14, 2015

DIWANI MTEULE WA KATA YA MOSONGO SERENGETI(CHADEMA)AANZA KUTEKELEZA AHADI KABLA YA KUAPISHWA


 Diwani wa kata Mosongo Samson Mrimi(Chadema)akimwangalia fundi baada ya kugharamia matengenezo ya kisima cha maji  Kenokwe ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyotoa kwa wananchi wakati wa kampeini kilichoharibika toka mwezi julai mwaka huu,picha zote ni kwa hisani ya Serengeti Media Centre


MITARO YA BARABARA YA MUGUMU MJINI SERENGETI YAENDELEA KUTESA MADREVA.

 moja ya gari lililokwama katika mtaro wa barabara inayojengwa kwa kiwango cha Lami Mugumu mjini,eneo hilo lililo karibu na hoteli ya Kirawira limegeuka kero kwa madreva wa magari,boda boda na watembea kwa miguu






Gari la hifadhi ya Taifa ya Serengeti likivutwa na Noah baada ya kukwama katika mtaro wa barabara ya Mugumu mjini inayojengwa na kampuni ya Samotta kwa kiwango cha lami.