Fahari ya Serengeti

Thursday, May 31, 2018

MAZISHI YA MWANAMKE ALIYEUAWA NA MPENZI WAKE

Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Merenga wilaya ya Serengeti wakimstiri Neema aliyeuawa na mpenzi wake kutoka na wivu wa mapenzi.
Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa Suzana ambaye alikuwa amemuoa Neema ndoa ya Nyumbanthobu.
Suzana aliyekuwa amemuoa Neema ndoa ya Nyumbathobu akiwa na wajukuu wake wawili walioachwa na mama huyo aliyeuawa na mpenzi wake kutokana na wivu wa mapenzi


Waombolezaji

Mwili wake ukipelekwa kaburini

Taratibu zinaendelea
Diwani Francis Garatwa akatoa ushauri wa watu kuacha matendo ya kuuana



Enzi zao mapenzi yakiwa motomoto



Thursday, May 24, 2018

WANAFUNZI SEKONDARI NYAMBURETI WATOA YAMOYONI

Ded Serengeti Juma Hamsini akijadiliana na wanafunzi wa sekondari ya Nyambureti juu ya changamoto zinazowakabili na mikakati ya halmashauri katika sekta ya elimu.
Anasisitiza wanafunzi hao kusoma na kuachana na mambo yanayowafanya washindwe kufikia matarajio yao na halmashauri inaendelea na mikakati ya kuboresha miundo mbinu ya elimu.
Anawapima uwezo kielimu

Mjadala jumuishi ukiendelea
Anasisitiza jambo mahsusi kwa wanafunzi mbele ya walimu na maafisa wengine.

UKAGUZI MAABARA ZA KISASA SEKONDARY

Ili kutengeneza wanasayansi wazuri halmashauri ya wilaya ya Serengeti imewekeza fedha nyingi katika kuboresha maabara kwa shule za sekondari.
Ukaguzi unaendelea ili kuhakikisha ukamilishaji wa kazi hiyo unafanyika kwa wakati na wanafunzi watakapofungua julai wakute maabara ziko tayari na vifaa  vyake.

Ufuatiliaji.

Ukaguzi unaendelea


Wednesday, May 16, 2018

USAFI KWA AFYA WAPUNGUZA MAGONJWA KWA WANAFUNZI MBIRIKIRI

Ofisa Michezo wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara Mayige Makoye akiongea na wanafunzi wa shule ya Msingi Mbirikiri kata ya Sedeko juu ya kutumia michezo kupeleka ujumbe kwa jamii Usafi kwa Afya ili kuhakikisha wanapiga vita magonjwa yanayosababishwa na uchafu.

Usafi kwa Afya ni Mradi unaotekelezwa kata za Kisangura na Sedeko chini ya shirika la amref health tanzania kwa ufadhili kutoka Spain

Maelekezo mbalimbali yakitolewa.

 Wanafunzi wakifuatilia maelekezo


 Wakiwasilisha michezo yao
 Wengine walipanda juu ya miti ili kuhakikisha wanaona yanayofanyika.



Tuesday, May 15, 2018

VIBUYU MCHIRIZI VYAIMARISHA USAFI SHULE ZA MSINGI

 Walimu,wazazi na baadhi ya maafisa wa Mradi wa Usafi kwa Afya unaotekelezwa na amref health tanzania wakiangalia kibuyu mchirizi katika shule ya Msingi Tabora B wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara ambavyo vimesaidia kuimarisha usafi wa wanafunzi watokapo chooni.
 Mwalimu Tabitha Mugini akitoa ufafanuzi kwa wanafunzi wa shule ya Msingi Tabora B umuhimu wa usafi wao,na mazingira yanayowazunguka kuwa ni kinga muhimu ya kuepuka magonjwa ya kuambukizwa yanayotokana na uchafu.
 Wanafunzi wanafuatilia maelekezo.
 Walimu Tabora B wakielezea mikakati yao.
 Ujumbe kwa njia ya nyimbo ulitolewa.
 Burudani toka kwa klabu ya mazingira
 Kibuyu Mchirizi nyenzo rahisi kwa usafi

Heshima ikatolewa