Fahari ya Serengeti

Friday, March 31, 2017

VIONGOZI WA VIJIJI ,DINI,SHULE NA KATA YA MBALIBALI WILAYANI SERENGETI WAJENGEWA UWEZO

 Mada mbalimbali zikitolewa na Paul Makuri mmoja wa wahitimu wa Shirika la FES ambalo limefadhili mafunzo hayo ambayo yanalenga jamii zilizoko pembezoni.
Mkaguzi wa ndani wa hesabu halmashauri ya wilaya ya Serengeti  JuliusNguruka akitoa mada kwa  viongozi wa vitongoji,vijiji,dini,walimu na wazee wa mila kata ya Mbalibali wilayani Serengeti ,juu ya utawala bora,ushirikishaji jamii na namna ya kutumia rasilimali zinazowazunguka kwa ajili ya kujiletea maendeleo,mafunzo yaliyoratibiwa na Shirika la Kijermani la Friedrick Ebarf Stiftung(FES) Tanzania ,lengo ni kuhakikisha jamii inashiriki katika mipango na kusimamia shughuli za maendeleo zinazotekelezwa katika maeneo yao.




Viongozi mbalimbali wakiendelea na semina
Dozi inazidi kuwaingia

KESI YA NGARIBA YAPIGWA TAREHE

SERENGETI MEDIA CENTRE
Ngariba Wansato Buruna kushoto akiwa mahakamani ,kulia ni mwenzake ambao wanashitakiwa kwa makosa ya kukeketa watoto.

Kushindwa kufika mahakamani kwa watoto ambao ni wanafunzi kumesababisha kesi  tano  za jinai zinazomkabili  Ngariba Wansato Buruna(56)na wenzake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara kuahirishwa.

Watoto ambao wanaendelea na mitihani kwa ajili ya likizo fupi walitakiwa na mahakama hiyo kuwasilisha ushahidi wao dhidi ya ukatili unaodaiwa kufanywa na ngariba huyo na wenzake  mwishoni mwa mwaka jana ambao walikeketwa na kisha kukamatwa na askari polisi na kuwataja washitakiwa kuwa ndiyo waliohusika.

Hata hivyo hakimu wa Mahakama hiyo Ismael Ngaile ameahirisha kesi hiyo hadi aprili 21 mwaka huu.

Aidha uamzi mdogo uliotakiwa kutolewa Katika shauri namba 234/2016 dhidi ya Wansato Buruna(56) na Bhoke Mseti(40) wanaotetewa na wakili Baraka Makowe haukutolewa hadi 

aprili 21 mwaka huu,na Mahakama imempa dhamana mshitakiwa  Bhoke Mseti baada ya kutimiza vigezo na masharti ya dhamana ya sh 5 milioni ya maneno na wadhamini wawili.

Mwisho.

SERENGETI MEDIA CENTRE: JELA MIAKA 30 KWA KUBAKA

SERENGETI MEDIA CENTRE: JELA MIAKA 30 KWA KUBAKA: Serengeti Media Centre. Joseph Nyiboha(22)mkazi wa kijiji cha Borenga wilayani Serengeti Mkoani Mara amehukumiwa kifungo cha miaka...

JELA MIAKA 30 KWA KUBAKA


Serengeti Media Centre.

Joseph Nyiboha(22)mkazi wa kijiji cha Borenga wilayani Serengeti Mkoani Mara amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela  kwa kosa la kubaka na kumpa mimba mwanafunzi aliyekuwa amechaguliwa na kujiunga na  kidato cha kwanza Machochwe sekondari.
Hata hivyo  mshitakiwa wakuwepo mahakamani kwa kile kinachodaiwa kuwa alitoroka baada ya kudhaminiwa.
Kabla ya kutolewa adhabu hiyo mwendesha mashitaka wa Jamhuri Jakobo Sanga Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa wilaya Ismael Ngaile  akisoma maelezo katika kesi ya jinai namba 87/2016 ,alisema mshitakiwa alifikishwa mahakamani akikabiliwa na makosa matatu ya jinai.
Alitaja kosa  la kwanza kuwa ni kuishi na mwanafunzi kinyume na kifungu 134 cha Sheria ya Elimu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, na kosa la pili ni kumbaka mwanafunzi wa miaka 15 aliyetarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza Machochwe sekondari 2016 ikiwa ni kinyume na kifungu namba 130(1)na(2)(e)na namba 131(1)cha sheria ya ubakaji sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Sanga aliiambia Mahakama kuwa kosa la tatu ni  kumpa mimba mwanafunzi kinyume na kifungu namba 35(3)na(4)sheria ya Elimu sura ya 353 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Mshitakiwa alikamatwa Oktoba 24 mwaka 2015 nyumbani kwake katika kijiji cha Borenga  baada ya kubainika kuishi na Mwanafunzi wa shule ya msingi Borenga aliyekuwa amechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza  Machochwe,hata hivyo alikuwa tayari ni mjamzito,na kuomba adhabu kali itolewe.
 Hakimu Ngaile alisema ushahidi  uliotolewa mahakamani haukuacha shaka”mahakama yangu inatoa adhabu kali kwa mshitakiwa ,katika kosa la kwanza atatumikia  kifungo cha miaka 5 jela, kosa la pili   kifungo cha miaka 30  jela na kosa la tatu atakwenda jela miaka 30 adhabu zote zitakwenda pamoja atatumikia miaka 30”alisema.
mwisho.

Thursday, March 30, 2017

JELA KWA KUISHI NCHINI BILA KIBALI


Serengeti Media Centre

Gari la Polisi likitoka mahakama ya wilaya kupeleka mahabusu ya Mugumu waliohukumiwa vifungo na mahabusu,Picha na Serengeti Media Centre.
.Mahakama ya Hakimu Mkazi wa  wilaya ya Serengeti mkoani Mara imemhukumu Julius Chacha(50)kifungo cha mwaka mmoja au kulipa faini sh 500,000 kwa kosa la kuishi nchini bila kibali.

Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Amaria Mushi alitoa hukumu hiyo baada ya kujiridhisha pasipo kuacha mashaka juu ya ushahidi  uliotolewa mahakamani hapo na upande wa Jamhuri ,huku mshitakiwa akishindwa kuwasilisha ushahidi na vielelezo vya uhalali wake wa kukaa hapa nchini.

Hakimu Mushi alisema mshitakiwa atatakiwa kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela iwapo atashindwa kulipa faini y ash 500,000,baada ya kutiwa hatiani kwa kosa moja aliloshitakiwa nalo la kuishi  nchini bila kibali kinyume na kifungu namba 31(1) na (2) sheria ya uhamiaji sura ya 54 mapitio ya mwaka 2002 Kama ilivyofanyiwa marekebisho  sheria namba 8 ya mwaka 2015,hata hivyo amepelekwa gerezani baada ya kushindwa kulipa faini.

Mapema mwendesha mashitaka wa Polisi Paskael Nkenyenge akisoma maelezo ya shitaka katika kesi ya jinai namba 164/2016 mbele ya Mahakama hiyo alisema,mshitakiwa alikamatwa agosti 31 mwaka 2016 eneo la mugumu mjini siku moja Kabla ya maandamano yaliyoandaliwa na chama Cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA)maarufu kama UKUTA. 

Alisema kabla ya kukamatwa Agosti 31 mwaka 2016 aliwahi kukamatwa oktoba 21,2015 kwa kosa kama hilo na kufikishwa  katika kituo  kidogo cha polisi  Natta ,hata hivyo alitoroka baada ya kupata dhamana na  hadi alipokamatwa  wakati wa maandalizi ya maandamano ya UKUTA.

Katika mahojiano ilibainika siyo mtanzania bali ni mzaliwa wa Nchi jilani ya Kenya yeye na mama yake mzazi Angelina Okinyi ,ingawa alidai baba yake ni Mtanzania lakini hakuweza kuwasilisha vielelezo vyovyote vinavyothibitisha madai yake.

Pia ilibainika mshitakiwa Julius alisoma katika Shule ya Msingi Kombe iliyopo kata ya Kihancha na elimu ya sekondari katika Shule Tarang'anya iliyopo nchini Kenya na alihitimu  mwaka 1991.

Wakati huo huo David Mwita(41)mkazi wa Mjini Mugumu wilayani Serengeti amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa wilaya ya Serengeti  Ismael Ngaile kwa makosa ya kupatikana na bangi kilo 13.7.

Mwendesha mashitaka wa Polisi Jakobo Sanga aliiambia mahakama hiyo kuwa mshitakiwa alikamatwa na askari Polisi machi 26 majira ya saa 4 asubuhi mwaka huu ndani ya basi akisafirisha bangi mbichi yenye uzito wa kilo 13.7 kwenda Nyamongo wilayani Tarime.

Alisema kosa la kwanza ni kupatikana na bangi kinyume na kifungu namba 15(1)(a)cha sheria namba 5 ya mwaka 2015 ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya,na kosa la pili ni kusafirisha bangi kinyume na kifungu namba 15(2) cha sheria namba 5 ya mwaka 2015 ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya.

Mshitakiwa alikana mashitaka na upelelezi umekamilika ,kesi hiyo itasikilizwa aprili 12 mwaka huu na mshitakiwa yuko mahabusu baada ya kukosa wadhamini.

Mwisho.

MWENYEKITI WA SERIKALI YA KIJIJI CHA BORENGA AKATALIWA NA WANANCHI

Wajumbe wa serikali ya kijiji cha Borenga kata ya Kisaka wilayani Serengeti wakiwa wamekaa chini ya mti hawana la kufanya kufuatia afisa mtendaji wa kata hiyo Mturi Sausi kuingia mtini baada ya kubaini kuna waandishi wa habari wanafuatilia sakata la Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Julius Maro kukataliwa na wananchi na yeye kutangaza kung'atuka lakini ameendelea kukalia ofisi huku akidaiwa kufanya hujuma mbalimbali ikiwemo uuzaji wa ardhi kwa wakazi wa Tarime.

Mtendaji huyo alikuwa ameitisha kikao cha Serikali ya kijiji kwa ajili ya kujadili mgogoro wao na mwenyekiti uliopelekea kumkataa mara mbili na kufuatiwa na mkutano mkuu wa kijiji kumkataa,hata hivyo baada ya kupata taarifa za uwepo wa waandishi wa habari kijijini hapo hakuweza kutokea na kusababisha wajumbe kukaa chini ya mti kwa muda mrefu wakimsubiri bila mafanikio.

Mkuu wa wilaya hiyo Nurdin Babu ameahidi kwenda kijijini hapo kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero hiyo ambayo imechangia shughuli za maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule kukwama kwa kuwa wananchi wamegoma kuchanga mpaka mwenyekiti awasilishe fedha zinazolipwa na mchimbaji mdogo wa dhahabu zaidi ya sh 6 mil,.

Jengo la shule ya Msingi Borenga ambayo imekwama kujengwa kutokana na mgogoro uliopo kati ya wananchi na mwenyekiti wa kijiji ,hata hivyo wananchi wanamtaka Mkurugenzi Mtendaji kupeleka mtendaji wa kijiji kwa kuwa maafisa kilimo wanaokaimu mara kwa mara wanadaiwa kuwa sehemu ya hujuma ya rasilimali za kijiji.
Baadhi ya wachimbaji wadogo wakiwa katika eneo lao la kazi ,mgodi huo unaodaiwa kuwa chini ya kijiji mchimbaji aliyeingia makubaliano na serikali ya kijiji anadaiwa hajalipa zaidi ya sh 6 mil,Mwenyekiti wa kijiji akidaiwa kumkingia kifua.

Tuesday, March 28, 2017

SINGITA GRUMETI FUND YAKABIDHI MRADI WA MAJI MTIRIRIKO

 Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu akikata utepe kama ishara ya kupokea mradi wa maji Mtiririko katika kijiji cha Iharara uliojengwa na Kampuni ya Singita Grumeti Fund kwa ushirikiano na Shule ya Sekondari ya Issenye na wananchi,kulia kwake ni Mkurugenzi wa Singita Grumeti Fund Steven Cuniliffe.

Mradi huo utakaonufaisha wakazi zaidi ya 3500,mifugo zaidi ya 2000 umegharimu zaidi ya sh 96 milioni ,Kampuni ya Singita Grumeti Fund ikiwa imechangia zaidi ya sh 82 milioni,sekondari sh 15 mil na wananchi zaidi ya sh 2.9 mil,utapunguza ukubwa wa tatizo la wananchi wa eneo hilo na wanafunzi waliokuwa wanaacha masomo kwa ajiili ya kutafuta maji.
 Picha ya pamoja baada yauzinduzi,kutoka kushoto ni afisa maendeleo ya jamii kampuni ya Singita Grumeti Fund Frida Molel,Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Iharara Goroban Mahega,Dc Nurdin Babu ,afisa mtendaji wa kijiji John Wangembe,afisa mtendaji wa kata ya Nagusi Molel na  Mkurugenzi wa Singita Grumeti Fund Steven

 Picha ya pamoja na wanafunzi wa Issenye sekondari katika eneo la matenki yanayopokea maji kutoka kwenye tenki kubwa kwa ajili ya matumizi ya shule.
 Mkuu wa wilaya akifungulia bomba kuhakikisha maji yanayotoka kwenye chanzo cha maji mtiririko kwa kutumia umeme wa mionzi ya jua.


 Afisa maendeleo ya jamii kampuni ya Singita Grumeti Fund Frida Mollel akitoa taarifa ya mradi.

 Pandeni miti kote huko Dk akitoa maelekezo




 Makamu Mkuu wa shule ya Issenye Ezekiel Onderi akitoa maelezo jinsi mradi utakavyowapunguzia wanafunzi na walimu umbali wa kutafuta maji.
 Mwenyekiti wa serikali ya Kijiji cha Iharara Goroban Mahega akishukuru kwa kupata mradi wa maji safi na salama kwenye kijiji chake na taasisi ya shule.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Serengeti William Makunja akihimiza wananchi kushikamana na wawekezaji ili waweze kutatua changamoto zinazowakabili.

 Dc anasaidni makabidhiano ya mradi


 Makabidhiano yamekamilika wanapongezana.
 Lango la kuingia katika chanzo kikuu cha maji eneo la mashambani linafunguliwa rasmi
Tunzeni miundo mbinu atakayehujumu atashughulikiwa kwa mjibu wa sheria.

Friday, March 24, 2017

BEI YA VYAKULA SOKO LA MUGUMU YAZIDI KUPAA

 Baadhi ya wauza nafaka za vyakula katika soko la mjini Mugumu wilayani Serengeti wakisubiri wateja,bei  ya mahindi kwa debe ni sh 25,000 hadi 26,000,mtama sh 30,000 ,na udaga ni sh 18,000.bei hizo zimepanda ndani ya wiki moja.

Wauza nafaka hao wanadai kuwa bei hizo zitazidi kupanda kutokana na kuadimika kwa chakula katika maeneo mengine.
 Biashara zinaendelea,


Sunday, March 19, 2017

MKUU WA MKOA WA MARA AKAGUA UJENZI WA MADARASA NA BWENI LA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk Charles Mlingwa akikagua ujenzi wa madarasa manne na bweni la watoto wenye mahitaji maalum shule ya msingi Mugumu wilayani Serengeti ambayo yanagharimu zaidi ya sh 245 mil.Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu.







 Shughuli za ujenzi zinaendelea.
 Rc Dk Mlingwa akitoa akielezea misimamo ya serikali kwa wananchi wa Robanda ikiwemo matumizi mazuri ya fedha zinazotokana na uhifadhi,kuacha kuingiza mifugo kwenye maeneo yaliyohifadhiwa.





Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa na bweni la watoto wenye mahitaji maalum shule yamsingi Mugumu Robert Ng'oina akitoa taarifa ya mradi huo baada ya mkuu wa mkoa kukagua mradi huo.Picha zote na Serengeti Media Centre.

Saturday, March 18, 2017

TANESCO WAAHIDI KUSAMBAZA UMEME MAENEO YOTE YA ROBANDA

Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco)wilaya ya Serengeti Mhandisi Magoti Mtani akitoa maelezo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk Charles Mlingwa kushoto jinsi walivyosambaza umeme katika kijiji cha Robanda kwa kupitia chini(Underground)na kuahidi kuwa ya kipaumbele kama Taasisi na wananchi yatapata umeme kwa haraka ili kuharakisha huduma na uzalishaji mali.
Meneja wa Tanesco Mhandisi Magoti Mtani kulia akiwaonyesha mfumo uliotumika kushusha umeme toka juu na hatimaye kushusha chini na kupeleka kijijini ,kushoto mkuu wa Mkoa wa Mara Dk Mlingwa na viongozi wengine wakifuatilia maelezo kwa kuangalia juu ya nguzo.
Ufafanuzi wa mtandao huo unaendelea.
Maelezo ya kitaalam yanatolewa.


Mhandisi Magoti kulia akimwongoza mkuu wa Mkoa wa Mara dk Mlingwa wa pili toka kushoto kuelekea eneo la mradi,wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa halmashauri Juma Porini na katikati ni Dc Nurdin Babu.
Rc dk Mlingwa akiwasili katika kijiji cha Robanda kwa ajili ya kukagua miradi,na mkutano wa hadhara wa kijiji ambapo baadhi ya malalamiko ni suala la Single Entry,mapato ya Wma kutowanufaisha wananchi,Tembo kula mazao na mifugo kuingizwa maeneo ya kambi za kitalii.
Anasikiliza kero.

Hatimaye waliagana katika ofisi ya mkuu wa wilaya.