Fahari ya Serengeti

Wednesday, March 21, 2018

UJENZI WA KITUO CHA AFYA WASHIKA KASI

 Dc Serengeti Nurdin Babu watatu kutoka kulia akiwa na baadhi ya viongozi wa wilaya hiyo baada ya kufanya ziara ya kustukiza kwa lengo la kufuatilia kazi ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Natta kupitia fedha zaidi ya sh 400 mil zilizotolewa na serikali.
 Anasisitiza ujenzi mzuri na kuwa hawatawavumilia mafundi na wasimamizi watakao kwenda kinyume na masharti yaliyowekwa.
 Mafundi wakiendelea na kazi
 Akina mama hawakubaki nyuma




WANAHITAJI MEZA YA KUUZIA VYAKULA

 Baadhi ya wauza viazi ,matunda na mboga nje ya soko la Mugumu wilaya ya Serengeti jioni hulazimika kutandika chini bila kuzingatia mahitaji ya kiafya,hata hivyo wanaomba Mamlaka ya mji mdogo kuharakisha ujenzi wa miundombinu ya eneo maalum la kutolea huduma hiyo muhimu kwa afya za walaji.
 Biashara inaendelea

 Biashara mchanganyiko inaendelea
Wanahitaji soko maalum

UANDIKISHAJI WA VYETI VYA KUZALIWA

Uandikishaji wa vyeti vya kuzaliwa ofisi ya afisa mtendaji wa kata ya Stendi Kuu wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara ukiendelea kama inavyoonekana.
Wananchi wakisubiri huduma ya kuandikisha watoto wenye umri wa  chini ya miaka mitano
Wanasubiri huduma


NGARIBA AMWAGA MANYANGA

Ngariba Esther Bhoke mkazi wa Kitongoji cha Nyamihuru Kijiji cha Kitarungu kata ya Nyansurura wilaya ya Serengeti amebwaga manyanga na kusalimisha mikoba yake ambayo imeteketezwa hadharani chini ya Mchungaji wa kanisa la Kmt Mugumu  Cliford Msyangi na kushuhudiwa na watu mbalimbali katika ofisi za amref health tanzania.
NgaribaEsther  kulia akiwa na ngariba mstaafu Christina Marwa
Mchungaji Msyangi akifafanua maandiko ya Mungu kuhusu dhambi ya ukeketaji kabla ya kumwongoza sala ya toba.
Mchungaji Msyangi akimwongoza ngariba aliyebwaga manyanga sala ya toba
Baadhi ya mikoba ya ngariba

Mikoba inateketezwa hadharani
wanateketeza mikoba
wanashuhudia mikoba ikiteketezwa


Meneja amref Godfrey Matumu akiongea na Mchungaji Msyangi ofisini mwake ,kushoto ni afisa mradi wa Tokomeza Ukeketaji Serengeti William Mtwazi.

Saturday, March 17, 2018

WAZIRI WA KILIMO AHIMIZA KILIMO CHA KISASA

Waziri wa Kilimo na Ushirika Dk Charles Tizeba amesisitiza kilimo cha pamba kisasa ili kuwaweza kupata mapato mazuri kuliko wanavyofanya hivyo sasa hivi.akizungumza na baadhi ya wakulima wa kitongoji cha Nyakitono na kijiji cha Makundusi wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara,amewataka kuhakikisha wanaunda vyama vya ushirika ili waweze kunufaika na pembejeo na uuzaji wa pamba zao.
 Anasisitiza kuzingatia utaalam


Wananchi wakifuatilia kwa makini maagizo ya Waziri Tizeba

Thursday, March 8, 2018

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI WAZEE WA MILA NA NGARIBA WAONYWA

 Katibu Tawala wilaya ya Serengeti Cosmas Qamara akitoa maelezo kabla ya kumkabidhi Ngariba Mstaafu Christina Marwa cherahani katika maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani yaliyofanyika kijiji cha Nyansurura,jumla ya vyerahani vinne vimetolewa na shirika la Matumaini Mugumu vikiwa na thamani ya sh 320,000.
 Das amesema wazee wa mila na ngariba watakaojihusisha na ukeketaji hawataachwa salama mwaka huu.
 Wp Sijali wa Dawati la Jinsia la Polisi akisisitiza wananchi kuwapa ushirikiano kuwafichua watu wanaojihusisha na ukatili wa kijinsia
 Das Serengeti  akimkabidhi ngariba mstaafu Christina Marwa Cherahani

 Mmoja wa watoto waliohifadhiwa kituo cha Matumaini akipata cherahani





 Meneja wa Mradi wa Tokomeza Ukeketaji Serengeti unaotekelezwa na amref health tanzania Godfrey Matumu akielezea jinsi ambavyo wamejipanga kukabiliana na wale watakaojihusisha na ukeketaji mwaka huu.