Fahari ya Serengeti

Friday, January 30, 2015

MATUKIO YA UCHAGUZI WA MKT/MAKAMU MAMLAKA YA MJI WA MUGUMU-SERENGETI.

 AFISA MTENDAJI WA MAMLAKA YA MJI MDOGO WAMUGUMU -SERENGETI MAGINA NYIGANDA AKITOA UFAFANUZI NAMNA YA UPIGAJI KURA.


 WAJUMBE VITI MAALUM WA MAMLAKA HIYO WAKILA KIAAPO KABLA YA KUANZA UCHAGUZI.


 TUMAINI NYAMHOKYA MWANASHERIA WA HALMASHAURI AKIONGOZA KIAPO
 KIAPO
 WANAAPA
 KIAPO
 WAJUMBE WAKIDUATILIA MAELEKEZO
 JOSEPH RHOBI MAGOIGA CUF ALIYEPATA KURA 17 DHIDI YA 18 ZA CCM
 MJUMBE
 ANAOMBA UFAFANUZI
 MASWALI KWA MGOMBEA
 MIONGOZO,TAARIFA ILIKUWEPO

 PIGENI KURA KWA UTARATIBU HUU,ANASEMA DAS
T

 MGOMBEA ANAOMBA KURA
 FANUEL MAGESA CCM NDIYE MKT WA MAMLAKA
 UPIGAJI KURA


 MKT WA MAMLAKA AKISHUKURU KWA KUCHAGULIWA
 MKT WA HALMASHAURI JOHN NG'OINA
 MARWA RYOBA MWENEZI CHADEMA WILAYA
Z

Tuesday, January 27, 2015

Mmoja afa wanne wajeruhiwa

mmoja wa majeruhi katika ajali iliyohusisha gari la kampuni ya Grumet Fund wakati wanatoka kazini ,mlango wa roli lililokuwa limewabeba ukafunguka ,mmoja amekufa na wanne wako hospitali  Teule ya wilaya ya Serengeti akisaidia na ndugu zake ,hata hivyo amepelekwa hospitali ya rufaa ya Bugando kwa matibabu zaidi.

USAFIRISHAJI MIZIGO

 NG'OMBE WAKIKATIZA MJINI MUGUMU WILAYA YA SERENGETI WAKIWA NA SHEHENA YA VITI NA BIA,TOFAUTI NA KULIMA HUTUMIKA PIA KUSOMBA MIZIGO
 USAFIRISHAJI



Mmoja afa wanne wajeruhiwa ajali ya roli

 Majeruhi Mussa Ramadhani mkazi wa kijiji cha Makundusi wilaya ya Serengeti akiwa hospitali Teule ya wilaya ya Nyerere akiuguza majeraha kufuatia ajali ya roli walilokuwa wamepanda la kampuni ya Singita Grumeti kufunguka mlango wa pembeni wakati likiwa mwendo kasi na kuanguka,mmoja kati yao amefariki.
 majeruhi
 Mmoja wa majeruhi
 Majeruhi
 Majeruhi huyo amepelekwa hospitali ya rufaa ya Bugando kwa matibabu zaidi kutokana na kuteguka nyonga ya kiuno
 Majeruhi akiwa na baba yake hospitali Teule ya Nyerere wilaya ya Serengeti

Sunday, January 25, 2015

RIPOTI MAALUM: Wanafunzi shule ya msingi washiriki ujangili




 
http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/1596856/data/43/-/appotyz/-/ico_plus.png
Wanyama aina ya swala wakiwa katika mawindo porini. Picha ya Maktaba. 
Na Mwandishi Wetu, Mwananchi

Posted  Decemba27  2014  saa 10:34 AM
KWA UFUPI
·         Utafiti huo unaonyesha kuwa kwa Shule ya Tamkeri ambayo inapakana na hifadhi ya Serengeti mahudhurio ya wanafunzi mwaka 2013, yalikuwa  ni asilimia 27 na mwaka huu ni asilimia 29, wakati Mugumu B ambayo ipo karibu na Mugumu mjini, mahudhurio yalikuwa mwaka 2013 asilimia 99 na mwaka huu ni asimilia 100.
Serengeti. Inawezekana likawa jambo ambalo siyo la kawaida, lakini ndiyo hali ilivyo ya ujangili nchini hivi sasa, baada ya kubainika kuwa baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari zilizopo kando kando ya hifadhi na mapori ya akiba Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wameacha masomo na kushiriki ujangili wa wanyamapori kwa ajili ya kujipatia kipato.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kwa muda mrefu unaonyesha kuwa wanafunzi wa shule za msingi wanaoshiriki ujangili huo ni wa kuanzia darasa la nne hadi la saba na kwamba kazi hiyo wanaifanya kwa baraka za wazazi wao.
Baadhi ya wazazi wa wanafunzi hao wameamua kuwapa baraka watoto wao kuingia kwenye hifadhi kuwinda wanyamapori ili wakikamatwa na maofisa wanyamapori wahurumiwe na kuachiwa kutokana na umri wao mdogo.
Shule za msingi na sekondari zinazokabiliwa na tatizo la utoro wa wanafunzi za Kata ya Sedeko, Mbalibali na Machochwe ambazo ziko kando kando ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Mapori ya Akiba ya Ikorongo na Gurumeti.
Uchunguzi wa gazeti hili uliofanywa katika maeneo hayo na kuthibitishwa na walimu, waratibu elimu, madiwani, waendesha mashtaka na wadau mbalimbali umebaini vitendo hivyo hufanywa kwa sababu mbalimbali.
Jinsi ujangili unavyofanyika
Chacha Joseph mkazi wa Kijiji cha Machochwe anasema kuna aina nyingi ya uwindaji unaofanywa na wanafunzi hao mojawapo ni wanafunzi kuwinda wanyamapori usiku wakiwa na ng’ombe wao ili kukwepa kuonekana na askari wa hifadhi. Anasema hufanya kazi mbili kwa wakati mmoja, moja kuwapatia malisho ng’ombe wao ambao hawana sehemu ya kuwalishia wakati wa mchana na kufanya kazi ya uwindaji.
 Uwindaji hufanywa kwa kutumia kurunzi kubwa yenye mwanga mkali na njia ya pili ya kuwakimbiza wanyamapori wakiwa katika makundi kuwaelekeza katika makorongo makubwa yaliyopo katika hifadhi hiyo ambako hutumbikia na kufa. 
Anasema wakiingia eneo la hifadhi huwaacha ng’ombe wakiendelea kula majani, wao huelekea ndani zaidi ya hifadhi kutafuta wanyamapori ambako hupatikana kwa wingi.
Chacha anasema kwa kutumia kurunzi maarufu kama ‘kombora’ wanafunzi hao wakiwa katika kundi la watu 10 hadi 15, wakiwaona wanyama kama vile swala, pofu, nyumbu huwafuata taratibu kisha kuwamulika ghafla na kurunzi hiyo, hivyo kutokana na mwanga wake kuwa mkali huwachaganya  na hivyo, kwa kutumia mbwa na mikuki huwashambulia na kuwaua.
Anasema njia hii ya uwindaji huwafanya waue zaidi ya wanyama watano kwa siku.
Hata hivyo, anasema kwa njia ya kuwinda kwa kuwafukuza wanyama kwa kuwaelekeza katika makorongo makubwa huua wanyama wengi zaidi.
Anasema njia hii huua zaidi ya wanyama 50 kwa mpigo kwa sababu wanyama wengi huwa katika makundi makubwa hiyo wengi hutumbukia na kufa.
Chacha anasema kazi hii hufanyika kuanzia saa 4.00 usiku hadi saa 10.00 alfajiri na kwamba wakati wakiua wanyama huwa pia wanawasiliana na wazazi wao kwa ajili ya kuratibu mtandao wa kuuza nyama hizo.
Nyama hizo huuzwa katika maeneo ya kijiji walichotoka vijana hao na kama wamepata nyingi huwa inasafirishwa kwa kutumia pikipiki usiku huo huo na vijana wakubwa kupelekwa maeneo mengine ya Tarime na Rorya na wakati mwingine huvushwa hadi nchini Kenya.
Ofisa wanyamapori
Ofisa Wanyamapori mstaafu, Julius Nyigesa naye anasema ujangili unaofanywa na watoto hao kama hautadhibitiwa utakuwa na madhara makubwa kwa kuwa wengi wao wanaacha ujangili wa nyama na kujikita kwenye ujangili wa tembo na faru.
Anasema kuna aina nne ya ujangili anaoufahamu unaofanywa na wanafunzi hao; ujangili wa kutumia kurunzi kubwa, mbwa, mitego na kukaa muda mrefu porini wakiwasaidia wazazi kuwinda tembo na wanyama wengine. 
“Kuna ujangili wa aina nne ninaoufahamu unaofanywa na hao watoto, wapo wanaotumia kurunzi kubwa, mbwa na mitego na kulala huko kwa muda mrefu ambao unawafanya wawe wazoefu porini kwa kuwa hubeba majukumu ya kupika, kusomba maji na kukausha nyama,” anasema.
Anasema baada ya muda watoto hao hutumiwa na majangili wakubwa kwa kuwa wanao uzoefu mkubwa na mapori hayo kwa kujua wanyama wa aina fulani wanapatikana wapi na kwa wakati gani na ulinzi ulivyo.
Sababu za kufanya ujangili
Nyigesa anasema watoto hao kila mmoja ana sababu za kujiingiza katika ujangili.
Wapo ambao wazazi wamezeeka hawawezi kuwahudumia hulazimika kwenda kuwinda ili wapate fedha, wapo ambao wanaingia baada ya kuona wenzao wanafanya ujangili wanapata fedha nyingi na wengine wanaingia ili waweze kupata fedha za michango mbalimbali ya shule.
Nyisega ambaye alikuwa askari wanyamapori Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti anasema taarifa za wanafunzi hao kufanya ujangili zinafahamika na wazazi wao ama walezi kwa kuwa hurejea nyumbani wakiwa na nyama na nyingine huuza na kununua mifugo kama mbuzi na ng’ombe.
Hata hivyo, watoto hao wakikamatwa hujitokeza na kudai kuwa hawakuwa wanajua.
Mstaafu huyo anasema wakati mwingine wazazi huwaficha maeneo mbalimbali ikiwamo Wilaya ya Tarime waliko na ndugu zao kisha hutoa taarifa kuwa watoto wao waliuawa ndani ya hifadhi.
Kutokana na mapato wanayopata wanafunzi wengi huamua kuacha kwenda shule.
Ofisa wanyamapori huyo mstaafu anasema wanafunzi wengi waliokuwa wakiwakamata kwa kujihusisha na ujangili wengi walikuwa wakikamatwa na kuchapwa viboko, kisha kuachiwa na wale ambao umri wao ni mkubwa walikuwa wanapelekwa mahakamani.
Wakuu wa shule wadai hali ni mbaya
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Machochwe, Edna Nyambina na Mkuu wa Sekondari ya Kitunguruma, Andrew Phares wanakiri kuwa ujangili na kilimo cha tumbaku umeathiri sana masomo kwa kuwa wanafunzi ndiyo hutumiwa.
Wanasema kuwa tatizo hilo linajulikana kwenye kamati za maendeleo za kata na wilaya kwa kuwa wakati wanyama wanapoingia kwa wingi hasa nyumbu utoro nao huongezeka.
Mwalimu mwingine ni Nyihita Chacha Nyihita ambaye mwaka jana alikuwa mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Michochwe, anasema sababu kubwa ya utoro katika shule hiyo ni wanafunzi kufanya kazi ya uwindaji wa wanyamapori na kilimo cha tumbaku.
Anasema wanafunzi ambao wanashiriki kazi ya uwindaji ni kuanzia darasa la tano hadi la saba.
“Utoro ni mkubwa mno, wanafunzi wengi wanashiriki kazi ya uwindaji na kilimo cha tumbaku na kuacha shule,” anasema.
Nyihita ambaye alihamishiwa Shule ya Msingi Kibeyo iliyopo Mugumu mjini Februari mwaka huu, anasema kazi ya uwindaji kwa wanafunzi wa shule za msingi inachochewa na wazazi ili wajipatie kipato.
Anasema baada ya kuona utoro unazidi kuongezeka aliwahi kushirikisha kamati ya shule kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo, lakini alikwama kwa sababu wazazi hawakumpa ushirikiano.
Nyihita anasema ujangili kwa wanafunzi katika eneo hilo umekithiri kiasi kwamba inafikia mahali hata wanafunzi wenyewe wanaoshiriki  kuwinda wanyamapori wanawapigia simu walimu kuwauzia nyama.
“Inashangaza wanafunzi ambaye haji shule miezi miwili anakupigia simu akikuambia ‘Mwalimu nina nyama hapa ya pofu au swala nikuletee kilo ngapi?” anasimulia mwalimu huyo.
Anashauri ili kumaliza utoro katika shule hizo wazazi wanapaswa kuacha kuwatumia wanafunzi katika kazi za ujangili kwa sababu mbali ya kuwachosha wasifike shuleni, pia wanapata fedha ambazo wanaona hakuna haja ya kwenda shule.
Madiwani
Diwani wa Kata ya Machochwe, Samwel Gibewa anadai kuwa watoto hao walifanya kazi hiyo zamani na kwa sasa hawafanyi ujangili, badala yake utoro mwingi unachangiwa na kilimo cha tumbaku, kwa kuwa wanatumiwa na wazazi ama watu wengine kwa gharama nafuu.
Naye Chacha Nyikera Diwani wa Kata ya Sedeco alikiri kuwepo kwa utoro mkubwa kwa wanafunzi wa shule za msingi na huchangiwa na mambo mengi, ikiwamo la ujangili wa wanyamapori, wazazi wenyewe kutokuwa na mwamko na elimu.
Mahudhurio shuleni
Utafiti uliofanywa na Shirika lisilokuwa la kiserikali la Hakielimu katika Shule za Msingi Tamkeri, Mbalibali, Mugumu B na Kambarage zilizopo kando ya Hifadhi ya Serengeti unaonyesha kuwa mahudhurio ya wanafunzi shule hizo yanatofautiana kulingana na shule ilivyo karibu na hifadhi.
Kwa shule ambazo zipo karibu na hifadhi mahudhurio ya wanafunzi ni mabaya kutokana na baadhi yao kushiriki katika ujangili usiku na hivyo kushindwa kufika shuleni.inaendelea.