Fahari ya Serengeti

Wednesday, July 19, 2017

RC MARA AKUTANA NA MADUDU MRADI WA CHUJIO LA MAJI MUGUMU

 Rc Mara Dk Charles Mlingwa akipanda juu ya chuji la maji Mugumu wilayani Serengeti kwa ajili ya kukagua,hata hivyo alikutana na madudu kwa kazi iliyokuwa imefanyika ya kusuka nondo ili kumwaga zege kuanza kufumuliwa kutokana na Mkandarasi Kampuni ya Pet Cooperation Ltd kujenga bila kuzingatia hitaji la mchoro.
Aidha mradi huo unaosimamiwa na Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Musoma(Muwasa)ulianza kujengwa mwaka 2015 machi na ulitarajiwa kukamilika septemba 2015,hata hivyo haujakamilika na Mkandarasi aliomba muda hadi juni 30 mwaka huu angekuwa amemaliza na kukabidhi.

Katika hali ya kushangaza Muwasa na Mhandisi wa Kampuni hiyo walimkacha Mkuu wa Mkoa baada ya kujua angetembelea mradi huo,hali iliyomfanya fundi wa Kampuni hiyo kujigeuza mhandisi na baada ya kubanwa akakiri kuwa yeye ni fundi na si Mhandisi.

Mkuu wa Mkoa ameagiza kukutana na Muwasa na Mhandisi wa Kampuni hiyo ana kwa ana ili watoe maelezo kwa nini mradi huo haujakamilika na sababu za kumkacha na kuacha shughuli zinaendeshwa na watu wasiokuwa na sifa stahiki.
 Fundi wa Kampuni ya Pet Clodatus Felix akijibu maswali baada ya kujitambulisha kuwa yeye ni Mhandisi ,hata hivyo alikiri kuwa yeye elimu yake ni kidato cha nne tu.

 Rc Dk Mlingwa akimcharukia fundi huyo aliyejifanya Mhandisi na kuwa kazi yao hairidhishi na wanawafanya wakazi wa Mji wa Mugumu kunywa maji machafu wakati serikali imeishalipa zaidi ya asilimia 65 ya fedha ya mradi ambayo ni zaidi ya sh 1.4 bil.
 Maswali yalimwelemea fundi
 Fundi akitoa maelezo ya changamoto wanazokutana nazo ikiwemo ni wasimamizi wa Mradi Muwasa kutochukua hatua kwa wakati hali ambayo inachangia kuwachelewesha baadhi ya maeneo.




 Hata hivyo baada ya kutorodhishwa na maelezo ya fundi akaamua kutoka huku akiacha maagizo wamtafute kabla ya kutoka serengeti
 Anashuka
 Dc Serengeti Nurdin Babu naye akishuka na kufuatiwa na Ded Serengeti Juma Hamsini
Wahenga walisema kupanda mchongoma si kazi ,kazi ni kushuka wanateremka kwa tahadhari

1 comment:

  1. Kutengemaa kwa mradi huu wa ujenzi wa chujio la maji katika bwawa la Manchila ni habari njema kwa wakazi wa mamlaka ya mji mdogo wa Mugumu na viunga vyake, tunaomba weledi wa hali ya juu kwa wahandisi wanaohusika katika hili__ Serengeti shall never die

    ReplyDelete