Mradi wa Chujio la Maji Mugumu wilaya ya Serengeti ambao Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk Charles Mlingwa alimwahidi Makamu wa Rais Samia Suluhu kuwa atakabidhiwa juni 30 mwaka huu,sasa ni pasua kichwa kutokana na msimamizi wa Mradi Muwasa kutokuonekana eneo la shughuli,huku mkandarasi akidai kuwa amekwamishwa na Muwasa kwa kutokumpa baadhi ya vipimo.
Chujio hilo lililoanza kujengwa machi 2015 kwa muda wa miezi sita ,sasa ni zaidi ya miaka miwili na kazi haijakamilika,
Mbunge wa Jimbo la Serengeti Marwa Ryoba akiongea na msimamizi wa Ujenzi upande wa Mkandarasi Kampuni ya Pet
Cooperatives Ltd Clodatus Felix ,ambaye anadai kuwa mradi huo unakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo mchoro na kutokupewa kipimo cha maji kwa wakati na Msimamizi wa Maradi,Muwasa.
Mbunge Marwa Ryoba akipata taarifa kwa msimamizi wa ujenzi Upande wa Mkandarasi kuhusu tenki la maji ambalo halijaanza kujengwa licha ya muda walioomba kwisha juni 30 mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk Charles Mlingwa akipata maelezo ya mradi huo machi 13 mwaka huu alipozuru eneo la mradi na kuahidiwa kukabidhiwa mradi juni 30 mwaka huu,hata hivyo mradi huo haujakabidhiwa na hakuna anayeeleza lini watakamilisha na kukabidhi.
Mhandisi Mshauri toka Muwasa Kajigili akimwelezea Mkuu wa Mkoa jinsi shughuli zinavyokwenda wakati na kuwa juni 30 mwaka huu watamkabidhi,hata hivyo kabla ya siku za kukabidhi mhandisi huyo alikwenda likizo na kazi haijakamilika.
0 comments:
Post a Comment