SERENGETI MEDIA
CENTRE.
Mara .Mkurugenzi
wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Musoma
Hawaju Said Gantala (42)amefikishwa katika mahakama ya wilaya Musoma kwa
Makosa 15 ya kughushi nyaraka na kujipatia sh 63,400,000 kinyume cha sheria.
Mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Karimu Mushi ,wakili wa Takukuru Mkoa wa Mara
Moses Malewo katika kesi ya Jinai namba 176/2017 aliliambia mahakama hiyo Kuwa
Mshitakiwa anakabiliwa na Makosa hayo ya kughushi kujipatia fedha kwanjia ya udanganyifu
na kuwasilisha nyaraka za kupotosha katika benki zaCrdb na NBC matawi ya
Musoma.
Alisema kwa kosa la kwanza hadi la tano Mshitakiwa
anakabiliwa na Makosa yakughushi nyaraka za kuingiziwa mshahara (salary slip)
za Septemba hadi desemba 2014 ,kughushi nyaraka za kuingiziwa mshahara wa
juni,Julai na Agosti 2016 kwa kuonyesha kwamba ni nyaraka halali kutoka MUWASA
huku akifahamu Kuwa si kweli.
Alibainisha kuwa katika kosa la sita Gantala ili hali akijua
kuwa si kweli aliwasilisha nyaraka za kuingiziwa fedha benki ya Crdb Tawi la
Musoma ambazo zilikuwa zikionyesha kuwa katika mwezi septemba na desemba 2014
mshahara wake ulikuwa sh 2,767,549 na kujipatia mkopo wa sh 30 mil kinyume cha
sheria.
Malewo aliiambia mahakama kuwa kosa la saba mshitakiwa katika kipindi cha juni,julai na agosti 2016
alijipatia mkopo wa sh 34,400,000 kutoka
Benki ya Nbc Tawi la Musoma kwa kutumia nyaraka za kuingiziwa mshahara(salary
slip) za uongo zikionyesha kwamba mshahara wake ni sh 2,636,179.82 kinyume cha
sheria.
Kwa kosa la 8 hadi 13 Gantala akijua ni kosa aliwasilisha
nyaraka zauongo za kuingiziwa mshahara
wa mtumishi katika benki ya Crdb na Nbc Matawi ya Musoma akidanganya kuwa ni
halali kutoka Muwasa na kujipatia jumla ya sh 63,400,000 toka benki hizo.
Kwa kosa la 14 Wakili huyo wa Takukuru alisema Gantala
alimlaghai Mkuu wa Idara ya Utawala MUWASA Brian D.Moshi kuweka saini hati za
kuingiziwa mshahara wa Mtumishi (Salary Slip)kwa miezi ya juni,julai na agosti
mwaka 2016 ili zionekane ni hati toka Muwasa.
Alifafanua kuwa alifanya hivyo wakati akijua kuwa si nyaraka
halali na zililenga kuzipotosha taasisi hizo za fedha kinyume cha sheria.
Katika shitaka la 15 mshitakiwa alimlaghai Issaya Maswi
Nyaibo mkuu wa idara ya fedha MUWASA na kutia saini hati za kuingizwa mshahara
wa mtumishi (Salary Slip)za kughushi kwa miezi ya septemba,oktoba na novemba
2014 ili zionekane ni hati halali toka Muwasa wakati akijua ni makosa.
Mshitakiwa amekana mashitaka hayo na yuko nje kwa dhamana ya
wadhamini wawili kila mmoja kwa kuwa na hati ya mali isiyohamishika yenye
thamani kama kiasi hicho na kesi hiyo itatajwa agosti 22 mwaka huu.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment