Fahari ya Serengeti

Monday, July 24, 2017

CRDB BANK YAAHIDI KUUNGANA NA WADAU KUTANGAZA UTALII WA NDANI

 Meneja wa Crdb Bank Tawi la Mugumu wilaya ya Serengeti Melkoir Mapunda akimwelezea Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu jinsi Bank hiyo ilivyojipanga kusaidiana na wadau mbalimbali kutangaza utalii wa ndani ili kusaidia jamii kutumia fursa hiyo kwa ajili ya kujipatia mapato yao.
Ili kuhakikisha fursa hiyo inanufaisha jamii ,benki hiyo ni miongoni mwa wadau waliochangia maonesho ya Serengeti Festival Culture yaliyofanyika kwa siku tatu mjini Mugumu,
Mapunda amesema jitihada kubwa zinatakiwa kuelekezwa kwenye utalii wa utamaduni ili kusaidia kunyanyua uchumi wa jamii na Taifa kwa haraka.



0 comments:

Post a Comment