Fahari ya Serengeti

Friday, July 31, 2015

CHANJO YA KICHAA CHA MBWA

 Baadhi ya watoto wakiwa wamekaa na mbwa wao wakisubiri wataalam kwa ajili ya chanjo ya kichaa cha mbwa zoezi limefanyika kwenye uwanja wa Sokoine mjini Mugumu wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara.
 Wanasubiri
 Kila mtu na mbwa wake
 Kama ilivyokuwa wakati wa BVR watu wanapanga mistari hali kadharika chanjo ya mbwa watu wanalazimika kupanga mistari kama inavyoonekana
 Amesheheni ulinzi kila upande kama inavyoonekana hapo.

 Ili kuepuka ugomvi kila mmoja analazimika kumshikilia kwa makini mbwa wake.
 Wamewadhibiti








Thursday, July 30, 2015

GIZ YATOA VIFAA KWA HALMASHAURI YA SERENGETI

Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara Naomi Nnko akiwa na wataalam wa halmashauri hiyo wakipokea msaada toka shirika la Kijermani (GIZ)linaloshughulika na masuala ya maliasili katika halmashauri hiyo
Mkurugenzi wa shirika la GIZ Afrika Mashariki Martin Miiller akikabidhi kifaa cha kupimia ardhi,Total Station Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo  chenye thamani ya sh 27.3 mil.kwa ajili ya kupima viwanja,na mipaka.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti Naomi Nnko akiwa ameshikilia Total Station,kulia Mkurugenzi wa shirika hilo Tanzania Regine Qualmann akijiandaa kumkabidhi mashine mbili za GPS.
Regine Qualmann akimkabidhi Ded Nnko Gps mbili kwa ajili ya idara ya ardhi zenye thamani ya sh 3,980,000
Shirika hilo limekabidhi Printer ya kisasa kwa ajili ya idara ya Maliasili
Ded na afisa ardhi na Maliasili wilaya Jonas Nestory wakiwa na Printer baada ya kukabidhiwa.




KUDHIBITI MIGOGORO YA WANYAMA NA WANANCHI IDARA YA WANYAMAPORI KUPEWA GARI,
Serengeti:Shirika la Kijermani linaloshughulika na masuala ya Maliasili Tanzania(GIZ) linatarajia kutoa gari ,trekta na vifaa vya doria kwa halmashauri ya wilaya ya Serengeti ili kudhibiti wanyama wanaovamia mashamba ya wananchi.
Afisa wa shirika Afrika Mashariki Martin Miiller akikabidhi vifaa vya kupimia ardhi,viwanja , Gps 2 na Printa ya kisasa vyenye thamani ya zaidi ya sh 32 milioni kwa halmashauri ya wilaya ya Serengeti jana,alisema lengo ni kuijengea uwezo wa kusimamia masuala ya ardhi,Maliasili kwa jamii.
Alisema ili kupunguza migogoro kati ya jamii na wanyama shirika lao linatarajia kuikabidhi halmashauri hiyo gari jipya na vifaa kwa ajili ya doria ,lengo likiwa ni kuendelea kulinda na kuhifadhi Maliasili hizo ambazo zinafaida kwa jamii na Taifa.
“Katika Ikolojia ya Serengeti tunafanya kazi katika wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara  na Ngorongoro Mkoa wa Arusha…lengo likiwa ni kuhakikisha ikolojia hiyo inalindwa na kuendelea kustawi,lakini kwa maeneo mengine tunafanya kazi katika sekta za afya,huduma ya maji kwa mikoa ya Tanga,Mbeya na Dar es salaam,”alisema.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa shirika hilo hapa Tanzania Regine Qualmann alisema wameishatoa magari manne manne  kwa hifadhi ya Taifa ya Serengeti ,shirika la Frankurt Zoological Society(FZS)na halmashauri ya Ngorongoro ,lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kulinda na kuhifadhi Maliasili hizo.
Akipokea msaada huo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Naomi Nnko alisema ,kupitia mpango huo itawasaidia kuboresha huduma kwa jamii ikiwa ni pamoja na kuboresha makazi yao kwa kujenga nyumba za kisasa.
Afisa wanyamapori halmashauri hiyo John Landoyan alisema msaada wa gari utawasaidia kutatua matatizo ya wananchi kwa wakati na kupunguza migogoro kati ya wahifadhi na jamii,kwa kuwa wamekuwa hawawezi kufanya doria kutokana na tatizo la gari na vifaa vya doria.
Akizungumzia umuhimu wa vifaa walivyokabidhiwa afisa ardhi na Maliasili wilaya Jonas Masingija alisema kifaa cha kupimia ardhi kitasaidia kupima vijiji na viwanja ili kupunguza migogoro ya mipaka kati ya wananchi na maeneo yaliyohifadhiwa.
Katika halmashauri hiyo shirika hilo limejikita katika kujenga uwezo kwa halmashauri na jamii kwa masuala ya Maliasili ,na utawala bora.
Mwisho.



Wakuu wa idara wakishuhudia makabidhiano hayo

Ded akiwa na GPS
Uongozi wa halmashauri ukiwapa zawadi viongozi wa GIZ baada ya kukabidhi vifaa vyenye thamani ya zaidi ya sh 31.8 milioni.
Hii ni zawadi tunayokutunuku watu wa serengeti





CHUO CHA UTALII SERENGETI

Meneja wa Sabora iliyoko chini ya Kampuni ya Singita Grumeti Reserves na Fund wilayani Serengeti Mkoa wa Mara Wilson Ogembo akifungua jengo la Utawala chuo cha Utalii Serengeti(SETCO)ambalo kampuni hiyo ilichangia sh 19.5 milioni,anayepiga makofi ni Kaimu Mkuu wa chuo hicho Samwel Peter.
Mara baada ya ufunguzi .

Wilson akijiandaa kukata utepe kwa ajili ya kufungua jengo hilo liweze kutumika
Anakata utepe


Wanachuo wa chuo hicho na walimu wakiwa wamekaa wakifuatilia matukio yanayoendelea ya ufunguzi wa jengo la Utawala.

Wanafuatilia
Samweli Mewama mjumbe wa bodi ya chuo hicho akifungua bahasha kutoa zawadi kwa mgeni rasmi baada ya kazi ya kuzindua jengo hilo.


Cheti maalum kwa kampuni ya Singita Grumeti Reserves na Fund kwa mchango wao mkubwa wa kuwezesha ujenzi wa jengo hilo.
Vinywaji na karanga zilikuwepo kwa wageni

Wilson akishukuru uongozi wa chuo hicho kwa kutambua mchango wao mkubwa walioutoa

Saturday, July 25, 2015

SINGITA GRUMETIRESERVES NA FUND YATOA VIFA VYA AFYA NATTA

Mganga wa zahanati ya Kampuni ya Singita Grumeti Reserves na Fund iliyoko Kata ya Natta wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara Francis Muruthi akitoa taarifa fupi kabla ya kukabidhi vifaa vya afya kwa kituo cha afya cha Natta.

Viongozi mbalimbali wa serikali na Kampuni hiyo waliohudhuria makabidhiano ya vifaa hivyo,mashine ya Oxygen na magodoro sita
Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho Busima akitoa maelezo ya kituo hicho kwa viongozi wa serikali .
Meneja raslimali watu wa kampuni ya Singita Grumeti Reserves na Fund Angela Msechu akitoa maelezo nini wanafanya kwa jamii katika kuboresha huduma za jamii.
Anasisitiza
Anasema msaada huo una thamani ya zaidi ya sh 5.7 milioni unalenga kuboresha huduma za afya katika kituo hicho.

Katibu Tawala wilaya ya Serengeti Cosmas Qamara akiangalia mashine ya Oksijen baada ya kukabidhiwa.
Asante sana ni kauli ya mganga mfawidhi wa kituo cha afya Natta Busima akimwambia Angela Msechu baada ya kukabidhiwa magodoro sita na mashine ya Oksijeni.
Katibu tawala anasaini hati ya makabidhiano
Angela anasaini pia hati ya makabidhiano.
Anasisitiza umuhimu wa kuboresha huduma za afya.