Fahari ya Serengeti

Saturday, July 11, 2015

DK KEBWE AMWAGA MSAADA WA VIFAA VYA AFYA JIMBONI

 Baadhi ya wafanyakazi wa hospitali Teule ya Nyerere wilaya ya Serengeti wakifungua kontena lenye vifaa vya afya ukiwa ni msaada wa dk Stephen Kebwe kwa hospitali hiyo na vituo vya afya,vifaa hivyo alivyopata kutoka shirika la Matter la Marekani  vina thamani ya zaidi ya sh 500 milioni
 Wanaendelea kufungua
 Vifaa mbalimbali ikiwemo viti vya wagonjwa vikishushwa kama inavyoonekana
 Kazi ya kushusha vifaa hivyo haikuwa ndogo kutokana na wingi wa vifaa.
 Watu wanaenda wakiongezeka kama inavyoonekana hapo.
 Vifaa mbalimbali vya kisasa vikiwa tayari vimeshushwa ambavyo vitasaidia kupunguza ukubwa wa tatizo la uhaba wa vifaa vya afya katika hospitali na vituo vya afya.
 kazi ya kusomba na kupanga haikuwa rahisi kutokana na wingi wa vifaa.
 Baadhi ya vifaa ,msaada huo ni awamu ya kwanza anasema bado kontena nne moja ikiwa ni kwa ajili ya vifaa vya chuo cha Uganga na Uuguzi cha Kisare.
 Wanahakiki kimoja baada ya kingine
 Uhakiki unaendelea kwa umakini huku kaimu mganga mkuu wa hospitali hiyo Emiliana Donald kulia anavyofuatilia.
 Jamani tusaidiane maana mzigo ni mzito,kama vitanda vya kisasa,Utra sound,Laptop kwa ajili ya kuhifadhi taarifa mbalimbali za wagonjwa na kumbukumbu zingine .
Waganga na wauguzi wakiwa wakiangalia vifaa.


 Kila, mmoja alishiriki kushusha na kusomba
 kazi inaendelea


 Dk Emiliana anasema tatizo la upungufu wa vifaa limepata mwarobaini
 Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha uuguzi na Ukunga cha Kisare wakiendelea na mazoezi
Mazoezi yanaendelea

Dk Kebwe akiangalia nyaraka mbalimbali za ujenzi wa hospitali ya halmashauri ya wilaya ya Serengeti inayoendelea kujengwa ,chumba cha upasuaji kimekamilika na baadhi ya vifaa vimeishaandaliwa
Bi Kyariga mtaalam wa maabara anayeishi Marekani mzaliwa wa kijiji cha Masinki Serengeti akiwaeleza wanachuo cha Kisare wajitahidi kusoma na wawe namalengo makubwa ,yeye ni kiungo kati ya dk Kebwe na Kampuni ya Matter ya Marekani ambayo imekubali kusaidia wilaya kwa kipindi cha miaka miwili vifaa vya michezo
Wakati wa kuwasili kwa kontena la vifaa hivyo kulivuta hisia za watu mbalimbali kwa kuwa suala la afya linagusa kila mmoja.
Shughuli ilikuwa kubwa na iliwapata wenyewe
Ikawa shamra shamra
Ni burudani kwa kuwa miongoni mwa mambo yanayochangia vifo vya wanawake wajawazito na watoto chini ya miaka mitano ni ukosefu wa vifaa na huduma za afya.
Dk Kebwe ni miongoni mwa watu waliokuwa wakiburudika
Mzigo unaingia unaingia
msafara wa gari hilo ulisindikizwa na askari wa usalama barabarani ambaye anasalimiana na Ded Serengeti Naomi Nnko ambaye alikuwa miongoni mwa waliofika kushuhudia.
Dk Kebwe akitoa maelezo juu ya vifaa vilivyomo ndani ,kushoto ni kaimu mganga mkuu wa wilaya Willy Mchonvu,Das Cosmas Qamara,Dc Ally Mafutah na Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali hiyo Emiliana Donald
Neema ,Neema anasikika akisema
Maelezo yanatolewa

Dk Emiliana Donald akitoa maelezo kwa wananchi kuhusu tatizo la upungufu wa vifaa lilivyopata nafuu.

0 comments:

Post a Comment