Fahari ya Serengeti

Saturday, June 24, 2017

VIKUNDI 30 VYA VIJANA NA WANAWAKE SERENGETI VYAJAZWA MANOTI

 Baadhi ya wanavikundi vya vijana na wanawake kutoka maeneo mbalimbali wilayani Serengeti wakiwa kwenye mafunzo ya namna ya matumizi ya fedha za mikopo ambayo inatokana na asilimia tano ya makusanyo.
Halmashauri ya wilaya ya Serengeti kupitia makusanyo yake ya ndani imetoa zaidi ya sh 222 mil kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2016/17 kwa vikundi vya wanawake na vijana.
 Mwezeshaji akiwajengea uwezo namna ya matumizi ya fedha za mikopo.
 Wanafuatilia mada



 Afisa vijana wilaya Isack Mwankusye akitoa ufafanuzi wa malengo ya mikopo na jinsi wanavyotakiwa kurejesha ili wengine waweze kunufaika.



MABINTI WA NYUMBA SALAMA WANG'ARA MPIRA WA MIGUU



Add caption



Add caption



















Thursday, June 22, 2017

KUIMARISHA UTAFITI SINGITA GRUMETI FUND WATOA GARI KWA TAWIRI

 Afisa Mahusiano Msaidizi wa Kampuni ya Singita Grumeti Fund David Mwakipesile kulia akiwa ameshikana mkono na Profesa Todd Michael Anderson kutoka Wake Forest University Kitengo cha Baolojia Winston -Salem ambaye ni mmoja wa watafiti Katika Kituo cha watafiti wa Wanyamapori Serengeti,kama ishara ya makabidhiano,kulia ni Mkuu wa Kituo cha Utafiti Serengeti Dk Robert Fumagwa,wa kwanza kushoto ni muikolojia wa Senapa Asheli Loishooki.
Singita Grumeti Fund wametoa gari hilo ili kuimarisha shughuli za utafiti katika ikolojia ya Serengeti ambayo ni uti wa Mgongo wa uhifadhi hapa nchini kutokana na umaarufu wake

Friday, June 16, 2017

WATOTO SERENGETI WALIA NA MILA KANDAMIZI

 Watoto wakiwa na mabango yenye ujumbe wa kulaani mila kandamizi wilayani Serengeti Mkoa wa Mara wakati wa maandamano ya siku ya mtoto Afrika iliyofanyika kiwilaya
 viwanja vya shule ya msingi Mugumu B,

 Wanafuatilia michezo na nasaha mbalimbali kutoka kwa viongozi wa wilaya ya Serengeti.
 Mabango yenye jumbe mbalimbali yalikuwepo.

 Maigizo yenye ujumbe kwa jamii na watoto yametolewa,wamesisitiza kuepuka ukatili wa kijinsia kwa watoto,ndoa za utotoni,ukeketaji na mimba kwa wanafunzi ili wapewe elimu.

 Viongozi mbalimbali wakijadiliana mambo wakati burudani zikiendelea.
 Katibu Tawala wilaya ya Serengeti Cosmas Qamara akikagua banda la vifaa mbalimbali vinavyotengenezwa na watoto waliokimbia kukeketwa na kuhifadhiwa katika kituo cha Nyumba Salama Mugumu Serengeti.
 Dc Serengeti Nurdin Babu akitoa hotuba ambapo amezitaka mahakama na Polisi kuharakisha kesi zinazohusiana na ukatili wa kijinsia ikiwemo mimba kwa watoto,ukeketaji,ndoa za utotoni,vipigo ,ulawiti,ubakaji ,kwa kuwa jamii inakata tamaa kwa jinsi zinavyoendeshwa kwa muda mrefu.


 Bonanza la michezo limefanyika kwa mpira wa miguu wasichana na wavulana.








 Zawadi zimetolewa kwa waliofanya vizuri.












 Wataalam wa mitambo wako kazini kuhakikisha mambo yanasikika vema.



 Mtoto huyo alipata dhoruba wakati wa maadhimisho hayo na kupoteza fahamu,hata hivyo alipata ahueni.