Fahari ya Serengeti

Saturday, July 23, 2016

LIGI YA UMOJA CUP IMARA FC NA BURUNGA KUUMANA LEO UWANJA WA SOKOINE

 Mpambano wa Imara Fc na Burunga kufanyika uwanja wa Sokoine mjini Mugumu wilayani Serengeti


DC Serengeti atoa siku tano chanzo cha maji cha zamani kianze kutoa huduma ya maji kwa hospitali na kwa jamii wakati wanarekebisha mfumo wa umeme manchira

 Dc Serengeti Nurdin Babu atoa siku tano kwa Mamlaka na idaraya maji kufufua chanzo cha zamani cha maji ili kianze kutoa huduma hospitali na kwa jamii wakati wanaendelea na marekebisho ya mfumo wa umeme kwenye pampu ya maji bwawa la Manchira.
Kwa mjibu wa agizo hilo lililotolewa julai 21 mwaka huu katika kikao cha pamoja na Ded na wataalam wa idara hiyo utekelezaji wake unatakiwa kukamilika julai 26 iwapo watashindwa kukamilisha hatua kali dhidi yao zitachukuliwa.
Ikimbukwe kabla ya chanzo cha bwawa la manchira mji wa mugumu na viunga vyake vilikuwa vikipata huduma ya maji kutoka kwenye vyanzo hivyo kwa kutumia mashine za dizeli na wakati na nyingine waliweka sola.




MAGETA FC YAZIDI KUFANYA MAANGAMIZI YAIBAMIZA BOKORE FC MABAO 5-0 LIGI YA UMOJA SERENGETI

 Mshambuliaji wa timu ya Mageta Fc mwenye jezi nyekundu akimtoka mlinzi wa timu ya Bokore Fc wakati wa mchuano wa ligi ya Umoja kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine Mjini Mugumu wilayani Serengeti,Mageta waliwashikisha adabu Bokore kwa kuwachabanga magoli 5-0
Wachezaji wa timu ya Bokore Fc wakipata maelezo kutoka kwa mwalimu wao wakati wa mapumziko.
 Wanapata nasaha ,hata hivyo waliambulia kichapo chja magoli 5-0

 Ni mshike mshike kipa wa Bokore Fc anawahi mpira hukummshambuliaji wa Mageta Fc akiwa tayari kwa lolote.




Wednesday, July 20, 2016

LIGI YA UMOJA CUP YAZIDI KUPAMBA MOTO UWANJA WA SOKOINE MUGUMU SERENGETI

 Timu ya Kibeyo Fc ikimenyana na Burunga Fc katika ligi ya Umoja Cup iliyoandaliwa na Serengeti Media Centre,Magoiga na Mageta mshindi wa Kwanza anapata Ng'ombe,wa pili mbuzi na wa tatu Mpira,katika mtonange huo Kibeyo waliibuka washindi kwa magoli 2-0.





BAADHI YA HUDUMA ZA MATIBABU HOSPITALI TEULE YA NYERERE ZASITISHWA KUTOKANA NA TATIZO LA MAJI

 Baadhi ya wagonjwa na ndugu zao wakilalamikia mfumo mbovu wa hospitali kuwatoza fedha wakati wakijua baadhi ya huduma za matibabu zimesitishwa kwa ukosefu wa maji.

HUDUMA HOSPITALI ZASITISHWA KWA KUKOSA MAJI.
Serengeti:Baadhi ya huduma  katika hospitali Teule ya wilaya ya Nyerere wilayani hapa Mkoa wa Mara zimesitishwa kutokana na ukosefu wa maji hali ambayo kama haitatatuliwa mapema huenda akasababisha madhara makubwa kwa jamii.
Takribani miezi mitatu hospitali hiyo inayotegemewa na wakazi zaidi ya 200,000 wa wilaya hiyo na nje ya wilaya haina maji kutokana na kuharibika kwa pampu,hata hivyo baada ya matengenezo  hawajapata huduma ya maji kwa kile kinachodaiwa kuwa wanatakiwa kurekebisha miundo mbinu yao ya  bomba na tenki.
Wakiongea kwa kukata tamaa baadhi ya wanaoguza wagonjwa walisema wanalazimika kununua maji,kwenda na shuka zao kwa kuwa za hospitali ni chafu na hazifuliwi, na vyoo vya wagonjwa vimetapakaa  kinyesi kutokana na kutokuwa na maji.
“Nimefika hapa saa 3 asubuhi na mgonjwa wangu akiwa na hali mbaya,hadi saa 8 arasili hakuna huduma ,wauguzi na waganga wanasema hawawezi kutoa huduma wakati hakuna maji ,maabara na chumba cha upasuaji bila maji hawawezi kutoa huduma,”alisema kwa masikitiko Marwa Nyakibari.
Grace Joseph ambaye ana ndugu yake aliyelazwa chumba cha wazazi alisema,wanalazimika kununua maji mjini ,hata hivyo kwa wale wasiokuwa na uwezo wa kununua wanakabiliwa na hali mbaya zaidi.
Mganga Mkuu wa hospitali hiyo Emiliana Donald alidai kuwa huduma zinatolewa kama kawaida ,hata hivyo alikiri kutokuwa na maji kwa muda mrefu,huku akigoma kutoa ufafanuzi wa tatizo hilo ambalo linaweza kusababisha magonjwa ya mlipuko.
Meneja wa Mamlaka ya Maji Mugumu(Muguwasa)Mhandisi Dickson Gideon alisema kwa mjibu wa sheria ya Maji namba 12 ya mwaka 2009 wao wanawajibika kufikisha maji kwa mteja kupandisha kwenye tenki ni wajibu wake,hivyo kuitaka mamlaka iwapandishie maji hadi juu kwa gharama zile zile ni hasara na watashindwa uendeshaji.
“Pamoja na kuwa na hitilafu kwa sasa kwenye Control Panel baada ya marekebisho na kusababisha huduma kusimama ili isiungue tumeagiza vifaa na wakati wowote tutafunga,lakini hospitali lazima wabadilishe miundo mbinu yao ili maji yaende juu na hizo ni gharama zao si mamlaka,”alisisitiza.
Wakati mganga mkuu wa hospitali akidai huduma zinaendelea kama kawaida ,baadhi ya wauguzi na waganga waliokutwa wamekaa nje ya maeneo yao ya kazi walisema ,taarifa za uongozi wao hazina ukweli kwa kuwa hawatoi huduma katika mazingira hayo ambayo yanaweza kuwasababishia magonjwa ya mlipuko.
“Shuka hazifuliwi,hakuna maji maabara ,chumba cha wazazi ,upasuaji ,mawodini na vyoo vimetapakaa vinyesi harafu kiongozi anasema huduma zinaendelea,kama zinaendelea kwa nini wagonjwa wanalalamika kutopata huduma,?”walihoji baadhi ya wauguzi.
Boniphace Magori mkazi wa kijiji cha Remung’orori alisema alimfikisha mgonjwa wake akiwa na upungufu wa damu na kukuta hakuna huduma,na baada ya kuomba uongozi ndipo akasaidiwa .
“Kuna hatari ya kupata magonjwa ya mlipuko hapa maana hali ni chafu sana,tunatoka vijijini kuja kupata huduma kumbe tunakuja kubeba matatizo mengine,wagonjwa hawaogi ,hakuna maji kwenye vyoo ,”alisema.
Magreth John alisema wananunua dawa,kitanda wanalipia na maji pia ,ndani ya mawodi harufu ni mbaya hapakaliki kwa kuwa hata maji ya kufanyia usafi wauguzi wanawanyang’anya wagonjwa walionunua.
Hata hivyo kwa muda wa siku tatu sasa mji huo hauna huduma ya maji ya bomba hali ambayo inawalazimu wananchi kutafuta maji kwenye visima mbalimbali vya asili ambavyo si safi na salama.
Mwisho.

 Moja ya choo cha wagonjwa kikiwa kimetapakaa vinyesi kutokana na ukosefu wa maji hali ambayo ianweza kusababisha magonjwa ya mlipuko kama hatua za makusudi hazitachukuliwa kwa haraka.



SERENGETI CULTURE FESTIVAL YAZINDULIWA

Mkurugenziwa Tanapa Allan Kijazi kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Serengeti Arts Group Paulina Boma wakati  akikagua mabanda ya wajasiliamali,taasisi za umma na binafsi wakati wa tamasha la Serengeti Culture Festival lililoandaliwa na Serengeti Culture Centre kwenye viwanja vya Right To Play mjini Mugumu wilayani Serengeti.
Baadhi ya watazamaji wakiwa juu ya mti wakifuatilia burudani mbalimbali zinazotolewa ndani ya eneo la michezo wakati wa tamasha la Serengeti Culture Festival.
Kijazi akikagua banda la Senapa.
Anatia sahihi kuthibitisha alifika kwenye banda hilo wakati wa tamasha hilo ambalo linajumuisha watu kutoka kona zote za nchi ya Tanzania ikiwemo vikundi vya burudani.
Hilo ni Banda la Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro ambao wanashiriki katika maonesho hayo ikiwa ni pamoja na kuelezea kazi wazifanyazo kwa jamii .
Akikagua banda la Takukuru wilaya ya Serengeti.
Analakiwa na mratibu wa Nyumba Salama Rhobi Samweli ambao licha ya kuwahifadhi watoto waliokimbia kukeketwa pia huwafundisha kazi mbalimbali za mkono na baadhi ya kazi hizo ndizo zimewasilishwa kwenye maonesho hayo.
Burudani zilikuwepo ,kikundi kutoka Butiama kilikuwa kivutio.
Mzunguko kwenye vibanda unaelekea mwisho.
Burudani,burudani ,burudani.
kazi inaenda ikiongezeka

Katibu Tawala wilaya ya Serengeti Cosmas Qamara akisisitiza jambo kwa wananchi kuhusu umuhimu wa tamasha hilo la kitamaduni.
Ilipofika wakati wa hotuba alisisitiza matumizi ya mila na desturi zilizo nzuri kwa ajili ya kukuza utalii wa ndani na nje.

Anasisitiza.
Ukaguzi unaendelea.

Thursday, July 7, 2016

KAZI YA KUFUNGA PAMPU BWAWA LA MANCHIRA IMEKAMILIKA NA SASA MAJI YAANZA KUTOKA MJINI

 Mafundi kutoka Muwasa na Muguwasa wakiwa kwenye mtumbwi wakisafirisha Pampu kuelekea eneo la kufunga katika bwawa la Manchira wilayani Serengeti,kazi hiyo ilifanyika kwa siku mbili hatimaye na kufaulu kuwasha mashine na maji kuanza kutoka katika baadhi ya maeneo Kwa zaidi ya miezi miwili mji huo ulikuwa unakabiliwa na tatizo la maji kufuatia Pampu hiyo kuungua na kulazimu wananchi kuchota maji kwenye visima mbalimbali,huku bei ya maji ikipanda kutoka sh 100 hadi 500 kwa dumu moja.
 Maandalizi ya kutandaza nyaya kwa ajili ya kufunga kwenye pampu yakiwa yanaendelea kama inavyoendelea.
 Kazi haikuwa rahisi kutokana na uzito wa pampu hiyo na nyenzo duni ,hapo wanaisogeza bwawani.
 Wakati mwingine walilazimika kushaurina njia za kufanya ili kuifikisha pampu eneo husika ambalo liko ndani ya bwawa na pana kina kirefu cha futi 8 hadi 9.
 Kazi ya kufunga inaendelea.
 Mtumbwi wa kienyeji umeandaliwa kwa ajili ya kusafirisha Pampu.

 Kuna haja ya kufanya usafi karibu na chanzo cha maji ili mazingira yawe safi.
 Kazi ya kusogeza pampu ilishirikisha kila mmoja hapo.


 Kazi ya kuinganisha kabla ya kwenda kuifunga ilifanyika.
 Ubunifu ulitumika wa namna ya kusafirisha pampu hiyo kama inavyoonekana.
 Kazi ya kupeleka pampu kwenye mtumbwi inaendelea.
 Baadhi ya mafundi wakiwa wanachunguza mtumbwi kabla ya kuweka pampu.


 Kazi inaendelea

 Safari inaendelea ingawa ilikuwa ni hatari kutokana na mtumbwi wa kienyeji walioutumia,na wakati mwingine chuma kilichokuwa kikitumika kama podo kuwa kifupi na kukosa mwelekeo.


 Hapo ilimlazimu mmoja wa mafundi kumsaidia nahodha
 Pamoja na mafundi kutumia mbinu mbalimbali kwenda eneo la kazi,hata hivyo ilishindana na kuishia njia kama inavyoonekana.
 Safari inaendelea huku baadhi wakishuhudia nini kitatokea.
 Nahodha kuna wakati aliteleza na kuanguka majini na kumlazimu mmoja wa mafundi kusaidia kuongoza mtumbwi huku yeye akitumia uzoefu wake kuogelea .





Life Jacket ziliwasaidia wengine kuogelea.