Fahari ya Serengeti

Friday, December 29, 2017

ILI KUEPUSHA AJALI BODABODA WATAKIWA KUFUATA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

 Mwenyekiti wa waendesha bodaboda  Serengeti Frank Nyanswi akiwaasa wenzake kufanya kazi kwa kuzingatia sheria ili kupunguza ajali zisizokuwa za lazima na itawasaidia kupunguza migogoro na askari wa usalama barabarani.
Amesema hayo wakati wa kufunga mafunzo ya usalama ya wiki mbili katika Chuo cha Ufundi Chipuka yaliyofadhiliwa na Mbunge wa Jimbo hilo Marwa Ryoba kwa gharama ya sh 2 mil,ili kuwawezesha kujifunza sheria za usalama barabarani na kupata vyeti vitakavyowawezesha kukata leseni,jumla ya bodaboda 160 wamefuzu mafunzo hayo.

 Kamanda wa usalama barabarani wilaya ya Serengeti Timosi Chikoti katikati akifuatilia mafunzo ya usalama barabarani kwa bodaboda,kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Chipuka John Ntera,kulia ni mkufunzi wa Mafunzo koplo Ameir Rakwe.


CHUO CHA UFUNDI CHIPUKA CHAWANOA BODA 160 SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

 Baadhi ya bodaboda wa Mugumu wilaya ya Serengeti wakiwa kwenye mafunzo ya vitendo baada ya kumaliza mafunzo ya nadharia katika chuo cha Ufundi Chipuka,jumla ya boda 160 wamefuzu mafunzo kwa ufadhili wa Mbunge wa Jimbo hilo Marwa Ryoba na wanatarajia kupata vyeti vyao hivi karibuni na kuwawezesha kwenda kukata leseni.
 Askari wa usalama barabarani akiongoza mafunzo kwa vitendo namna ya kufuata sheria hasa maeneo ya muungano wa barabara.
 Wakiwa darasani wakifuatilia mafunzo
wanafuatilia kwa makini

Thursday, December 28, 2017

NGARIBA NGULI AFUNGWA MIAKA 8 NA MWENZAKE MIAKA 4

Ngariba Nguli Wansato Bruna (56)mkazi wa kijiji cha Rung'abure wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara kushoto amehukumiwa kifungo cha miaka 8 leo kwa makosa ya kuwakeketa watoto wa kike kinyume cha sheria

Monday, December 25, 2017

 Paroko wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Fransisco wa Asizi Mugumu wilaya ya Serengeti Joel Marwa akitoa Sakramenti ya Ubatizo kwa watoto 21 katika misa ya mchana ya Noel.
 Anapata sakramenti ya ubatizo





WASHINDI WA BONANZA LA MPIRA WA WAVU WABEBA SODA

 Wadau mbalimbali wamejitokeza kutoa zawadi kwa ajili ya washindi wa bonaza la mpira wa wavu Mugumu wilaya ya Serengeti,mchezo huo kwa sasa unashika kasi kwa kujizolea mashabiki wengi.
 Viongozi wakitoa maelekezo mbalimbali baada ya kumaliza bonanza ambalo lilikutanisha wachezaji wa timu hiyo na kuunda jumla ya timu nne.
 Wakiwa na zawadi zao

 Furaha ya ushindi

 Timu iliyokuwa ya tatu katika bonanza hilo

BONANZA LA MPIRA WA WAVU MUGUMU LAFANA

 Wachezaji wa timu ya mpira wa Wavu Mugumu wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara wakimenyana katika bonanza la sikukuu ya Krismas katika Uwanja wa Nhc mjini Mugumu.
 Mpambano unaendelea
 Mchezo huo kwa sasa umeshika kasi kwa mjini Mugumu kufuatia vijana wengi kujitokeza kucheza na kuvuta mashabiki wengi
 Wanafuatilia mpambano


Sunday, December 24, 2017

PILIKA PILIKA ZA KRISMASI MUGUMU


Biashara ya kuku kwa kipindi hiki cha sikukuu ya krismasi imeshika kasi katika mji wa Mugumu wilaya ya Serengeti kama inavyoonekana ,kuku mmoja huuzwa kati ya sh 10,000 hadi 15,000

 Biashara ni matangazo wanazunguka mtaani kusaka wateja

Chukua huyu ndiye bomba wakati wa sikukuu inaonekana ndivyo wanavyomshawishi mnunuzi



WAISHIO MAZINGIRA MAGUMU WAKUMBUKWA WAKATI WA SIKUKUU YA KRISMASI

 Juma Karamba kwaniaba ya Buiskol Luiser(Mama cheza)raia wa Uholanzi akigawa msaada wa mchele,maharage na fedha kwa watoto 145 waishio katika mazingira magumu Mugumu wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara kwa ajili ya sikukuu ya krisimasi,msaada huo wa zaidi ya sh 1,4 milioni ni mwendelezo wa kusaidia kundi hilo toka mwaka 2015 wakati wa sikukuu ya krismasi.

 Msaada ukitolewa


 Wakipata fedha


 Kila mtoto alipewa mbali na mchele kilo tatu ,maharage kilo tatu walipewa sh 10,000 kwa ajili ya kununua mahitaji mengine


 Wakisibiri kupata msaada
Rebeka kutoka mtaa wa MCU akiwa na wanawe watatu wakipata msaada huo,hiyo ndiyo dini ya kweli

Thursday, December 21, 2017

KATIKA KUBORESHA MAZINGIRA YA KUJIFUNZIA MBUNGE ATOA MIFUKO 250 YA SARUJI

 Mbunge wa Jimbo la Serengeti Marwa Ryoba kulia akimkabidhi mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Mesaga mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa,lengo ni kuboresha mazingira ya watoto kujifunzia na kufundishia.

Pia ametoa mifuko 50 Kenyamonta,Remung'orori(50)na Hekwe mifuko 100 ya saruji,hata hivyo amewataka wananchi kufanya kazi za maendeleo ili kuwawezesha watoto kupata mazingira mazuri ya kusoma,na kuwa waachane na wanaokwamisha maendeleo kwa misingi ya kisiasa,kwa kuwa hakuna atakayekuja kuwaboreshea Miundombinu ya shule zaidi ya wao wenyewe.
 Akiwasikiliza wananchi wa kijiji waliomsubiri barabarani baada ya kupata taarifa za ziara yake.

 Diwani wa kata ya Magange George Mahemba akielezea mikakati ya kata yao katika kuboresha miundombinu ya elimu .
 Anakabidhi kijiji cha Remung'orori saruji mifuko 50
 Anaongea na wananchi wa Nyagasense.

Wananchi wanafuatilia maelezo ya mbunge wao.

Tuesday, December 12, 2017

ROBANDA WAITIKIA MKAKATI WA JENGA HOSPITALI KWA SH 1000

 Dc Serengeti Nurdin Babu akifafanua jinsi wananchi wa wilaya hiyo wanavyotakiwa kuchangia ujenzi wa hospitali ya wilaya ambayo inatarajiwa kuanza kutoa huduma mwaka kesho januari,ili kukamilisha kazi hiyo kila mkazi wa wilaya hiyo anatakiwa kujenga hospitali kwa kuchangia sh 1000,hata hivyo wakazi wa kijiji cha Robanda wameahidi kuvunja rekodi ya kuchangia ili kufanikisha kupata fedha zaidi ya sh 1 bil kwa ajili ya kazi hiyo.
 Mrobanda Japan mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Robanda amesema,wananchi wako tayari kuchangia ujenzi wa hospitali hiyo kwa kuchangia ,mifugo,fedha na vitu vingine.
 Wananchi wanafuatilia mkutano huo
wanafuatilia