Fahari ya Serengeti

Friday, December 29, 2017

ILI KUEPUSHA AJALI BODABODA WATAKIWA KUFUATA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

 Mwenyekiti wa waendesha bodaboda  Serengeti Frank Nyanswi akiwaasa wenzake kufanya kazi kwa kuzingatia sheria ili kupunguza ajali zisizokuwa za lazima na itawasaidia kupunguza migogoro na askari wa usalama barabarani.
Amesema hayo wakati wa kufunga mafunzo ya usalama ya wiki mbili katika Chuo cha Ufundi Chipuka yaliyofadhiliwa na Mbunge wa Jimbo hilo Marwa Ryoba kwa gharama ya sh 2 mil,ili kuwawezesha kujifunza sheria za usalama barabarani na kupata vyeti vitakavyowawezesha kukata leseni,jumla ya bodaboda 160 wamefuzu mafunzo hayo.

 Kamanda wa usalama barabarani wilaya ya Serengeti Timosi Chikoti katikati akifuatilia mafunzo ya usalama barabarani kwa bodaboda,kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Chipuka John Ntera,kulia ni mkufunzi wa Mafunzo koplo Ameir Rakwe.


0 comments:

Post a Comment