Fahari ya Serengeti

Thursday, December 21, 2017

KATIKA KUBORESHA MAZINGIRA YA KUJIFUNZIA MBUNGE ATOA MIFUKO 250 YA SARUJI

 Mbunge wa Jimbo la Serengeti Marwa Ryoba kulia akimkabidhi mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Mesaga mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa,lengo ni kuboresha mazingira ya watoto kujifunzia na kufundishia.

Pia ametoa mifuko 50 Kenyamonta,Remung'orori(50)na Hekwe mifuko 100 ya saruji,hata hivyo amewataka wananchi kufanya kazi za maendeleo ili kuwawezesha watoto kupata mazingira mazuri ya kusoma,na kuwa waachane na wanaokwamisha maendeleo kwa misingi ya kisiasa,kwa kuwa hakuna atakayekuja kuwaboreshea Miundombinu ya shule zaidi ya wao wenyewe.
 Akiwasikiliza wananchi wa kijiji waliomsubiri barabarani baada ya kupata taarifa za ziara yake.

 Diwani wa kata ya Magange George Mahemba akielezea mikakati ya kata yao katika kuboresha miundombinu ya elimu .
 Anakabidhi kijiji cha Remung'orori saruji mifuko 50
 Anaongea na wananchi wa Nyagasense.

Wananchi wanafuatilia maelezo ya mbunge wao.

0 comments:

Post a Comment