Fahari ya Serengeti

Thursday, May 26, 2016

MAJI NA SUKARI PASUA KICHWA KWA WAKAZI WA MJI WA MUGUMU SERENGETI

MAJI SUKARI YAWATESA WAKAZI WA MJI WA MUGUMU
SERENGETI MEDIA CENTRE
Wakazi wa Mji wa Mugumu wilayani hapa Mkoa wa Mara wanakabiliwa na ukosefu wa maji safi kwa zaidi ya wiki mbili kufuatia mtambo wa kusukuma maji kutoka bwawa la Manchira kuungua.
Wakati sukari ikiuzwa  kati yash 3000-hadi 3500 kwa kilo na ikitolewa Nchini Kenya kwa njia za panya,ndoo ya maji imepanda kutoka sh  100 kwa maji ya bomba hadi sh 500 kwa maji ya shimoni na visima ,hali ambayo inazidisha makali ya maisha kwa wananchi na ni tishio la ongezeko la magonjwa yanayosababishwa na maji..
Baadhi ya wakazi wa mji huo walisemalicha ya maji waliyokuwa wanapata kutoka bwawa la Manchira kutokutibiwa  lakini yalikuwa yanapatikana kwenye mabomba kwa wakati wote na kwa gharama nafuu,ukilinganisha na hali ilivyo sasa ambapo wengi wanalazimika kuamka alfajiri kwenda kutafuta kwenye visima vya watu.
Meneja wa Mamlaka ya Maji Mugumu Dickson Kasese akiongea na Serengeti Media Centre kwa njia ya simu   alidai kuwa mtambo wa kusukuma maji umeungua kutokana na hitilafu ya umeme na kuwa zinatakiwa zaidi ya sh 180 mil za kununua mwingine.
“Inahitajika Pampu mpya maana Control Panel,Cable ya kuendesha motor zote zimekufa,tatizo hilo limebebwa na Mamlaka ya Maji Musoma ,na mtambo huo hapa nchini hakuna wameagiza nje ,itachukua zaidi ya wiki nne,tunatarajia mwishoni mwa mwezi juni au mwanzoni mwa julai  kama hatutapata njia  nyingine ya dharura,”alisema.
Alisema kwa sasa yuko Dar es Salaam wizara ya Maji ili kuwasilisha ombi la kupata mtambo mwingine utakaosaidia kutoa huduma kwa wananchi,hata hivyo alisema maelezo yao yanadai kuwa hawana mpaka waagize  nje na hautapatikana kwa muda mfupi kwa kuwa mpaka watengenezewe kiwandani.
Consolatha John,Esther Magige wakazi wa mtaa wa NHC mjini Mugumu walisema kuwa maji wanayouziwa kwa  sh 500 ni ya kwenye madimbwi ambayo yametuama wakati wa mvua,hivyo kama tatizo hilo halitapata ufumbuzi wa haraka huenda kukaibuka magonjwa ya mlipuko chanzo kikiwa maji.
Baadhi ya taasisi zilizokwishaanza onja adha ya ukosefu wa maji ni  pamoja na hospitali Teule ya Nyerere,gereza mahabusu,Kituo cha Nyumba Salama ,Machinjio  na wafanyabiashara wa nyumba za kulala wageni,migahawa na hoteli ambazo zilitegemea maji ya bomba kutoka bwawa la Manchira.
Hata hivyo baadhi ya wauza maji walisema kwa sasa wanapata faida kubwa nakudai kama matengenezo yatachukua muda mrefu wanategemea bei ya maji itapanda kwa kuwa hitaji litakuwa kubwa.
Mwisho.


 Baadhi ya wakazi wa Mtaa Mwema mjini Mugumu wakichota maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali katika kisima cha Chakuburya,






 Baadhi wa kazi wa mji wa Mugumu wakichota maji kwenye mtaro wa barabara eneo la Mkuu wa wilaya kwa ajii ya matumizi ya nyumbani,maji hayo ambayo si safi na salama.


Saturday, May 21, 2016

ZAIDI YA SH 111 MILIONI ZACHANGWA KUTENGENEZA MADAWATI SERENGETI


 
Serengeti Media Centre.
Zaidi ya sh 111 milioni zimechangwa na wadau mbalimbali wa maendeleo wilayani hapa Mkoa wa Mara kwa ajili ya kutatua changamoto ya upungufu wa madawati 16,000 kwa shule za Msingi na Sekondari.
Michango hiyo imetolewa na wadau wa maendeleo wakati wa kikao cha kuweka mikakati ya namna ya kutatua changamoto ya ukosefu wa madawati kwa shule za Msingi na sekondari ,ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dk John Magufuli la kuhakikisha tatizo la madawati linakwisha kufikia juni 30 mwaka huu kwenye ukumbi wa Giraffe Garden mjini hapa.
Mkuu wa wilaya hiyo Maftah Ally alisema baada ya kuguswa na matatizo yanayowakabili wanafunzi wa shule za msingi na sekondari na kuamua kuchangia fedha taslimu 3,313,000,ahadi za fedha sh 50,540,000 na ahadi ya madawati 477 kutoka kwa wadau mbalimbali.
“Kikao hiki kilikuwa cha kuweka mikakati ya kupata sh 2 bilioni kwa kupata madawati 14,594 kwa shule za msingi,meza 2,259 na viti 2,689 kwa shule za sekondari , wadau baada ya kuona ukubwa wa tatizo wakaamua kuchangia kiasi hicho,”alisema.
Mbunge wa jimbo hilo Mwalimu Marwa Ryoba aliyechangia madawati 100 yenye thamani y ash 12 mil,alisema shule nyingi zinakabiliwa na matatizo ya ukosefu wa madawati,hali ambayo inachangia kushuka kwa taaluma na ufaulu.
“Ofisi yangu imetoa imetoa madawati 100 kwa kuanzia na tutaendelea kuchangia ili tuhakikishe watoto wetu hawakai chini,na kitakachofuata ni vyumba vya madarasa,baada ya hapa tutawaunganisha wana Serengeti waioshio nje ya mkoa huu waweze kuchangia maendeleo ya wilaya yao,”alisema.
Mhifadhi wa Ujilani Mwema wa hifadhi ya Taifa ya Serengeti Nuhu Daniel alisema Tanapa imetoa sh 154 mil kwa wilaya nane zinazopakana na hifadhi hiyo na kila moja imepata zaidi ya sh 18 mil kwa ajili ya madawati,”pia tumetengeneza madawati 30 kwa ajili ya shule ya msingi Fort Ikoma,na tutaendelea kusaidia jamii inayotuzunguka kama ilivyo sera yetu,”alisema.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Juma Porini alisema halmashauri yake imetenga sh 100 milioni kwa ajili ya kutengeneza madawati,hivyo mchango huo wa wadau utasaidia kupunguza ukubwa wa tatizo na kuwataka wadau wanaowazunguka  washirikiane kusukuma mbele maendeleo ya wilaya hiyo.
Mkurugenzi wa Kibo  Safari’s Willy Chamburo ambaye anaendesha biashara ya utalii maeneo mbalimbali ikiwemo Serengeti alichangia madawati 50 yenye thamani ya Sh 6 milioni na kuwataka wafanyabiashara wa wilaya hiyo kuhakikisha wanashimana ili kuwajengea mazingira mazuri ya maisha watoto wao.
Baadhi ya wadau mbalimbali waliochangia ni pamoja wawekeza wa sekta ya utalii,wafugaji,wasanii,bodaboda,wakulima,Serengeti Media Centre,Ikona Wmas ,wafanyabiashara,Benki za Nmb,Crdb,Posta  na watumishi wa idara mbalimbali za umma.
Wilaya hiyo ina shule za msingi 110 za serikali zenye jumla ya wanafunzi 76302,sekondari 21 zenye wanafunzi 9359,inakabiliwa na upungufu wa madawati 14,594 kwa shule za msingi na sekondari meza 2259 na viti 2,689.
Mwisho.

 Igizo la kikundi cha Nyota Njema liliwakonga nyoyo wadau waliohudhuria kikao cha kuweka mikakati ya maendeleo ambacho kilizaa harambee ya zaidi ya sh 111 milioni.






 Mnada wa ng'ombe ulifanyika kwa ajili ya kukusanya fedha za utengenezaji wa madawati


 mijadala mbalimbali inaendelea nje ya Ukumbi

 Mnada wa Dvd ulifanyika ili kukusanya fedha za madawati





















Dc Maftah Ally akitoa taarifa ya makusanyo na nini kitaendelea baada ya hapo ili kuhakikisha wanakamilisha kazi ya madawati

Saturday, May 7, 2016

MKUU WA MKOA WA MARA AKIKAGUA BARABARA INAYOJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI MJINI MUGUMU


 Mkuu wa Mkoa wa Mara Magesa Mulongo aliyekanyaga juu ya daraja wakiwa na wataalam ,madiwani na wadau mbalimbali wakiangalia moja ya daraja kwenye barabara ya kilometa tatu  inayojengwa kwa kiwango cha lami na kampuni ya Samota Ltd kwa gharama ya sh 1.2 bilioni kutoka mfuko wa barabara,
Barabara hiyo ilitakiwa kukabidhiwa mei 6 mwaka huu kwa mjibu wa mkataba ,hata hivyo kazi hiyo haijakamilika,kutokana na kusua sua kwa kazi hiyo Mkuu wa Mkoa ameunda kikosi maalum cha uchunguzi ambacho kitatoa taarifa ndani ya wiki moja ili kubaini wanaochangia kukwama kwa mradi huo waweze kuchukuliwa hatua

 Mhandisi wa wilaya ya Serengeti Sospeter Leonidas mwenye karatasi akitoa taarifa kwa mkuu wa Mkoa wa Mara juu ya utekelezaji wa ujenzi wa barabara ya lami
 Wahandisi kutoka Tanrod na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wakiangalia BOQ ya mradi wa barabara
 Ukaguzi unaendelea
 Hapo wanaangalia mtaro ambao unadaiwa kujengwa kwa kutumia mawe chepechepe ambayo hupukutika yenyewe ikiwa ni kinyume cha mkataba
 Ukaguzi wa daraja
 Mjadala unaendelea kuhusiana na daraja hilo lilivyojengwa