Serengeti Media Centre.
Zaidi ya sh
111 milioni zimechangwa na wadau mbalimbali wa maendeleo wilayani hapa Mkoa wa
Mara kwa ajili ya kutatua changamoto ya upungufu wa madawati 16,000 kwa shule
za Msingi na Sekondari.
Michango
hiyo imetolewa na wadau wa maendeleo wakati wa kikao cha kuweka mikakati ya
namna ya kutatua changamoto ya ukosefu wa madawati kwa shule za Msingi na
sekondari ,ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dk John Magufuli la
kuhakikisha tatizo la madawati linakwisha kufikia juni 30 mwaka huu kwenye
ukumbi wa Giraffe Garden mjini hapa.
Mkuu wa
wilaya hiyo Maftah Ally alisema baada ya kuguswa na matatizo yanayowakabili
wanafunzi wa shule za msingi na sekondari na kuamua kuchangia fedha taslimu
3,313,000,ahadi za fedha sh 50,540,000 na ahadi ya madawati 477 kutoka kwa
wadau mbalimbali.
“Kikao hiki
kilikuwa cha kuweka mikakati ya kupata sh 2 bilioni kwa kupata madawati 14,594
kwa shule za msingi,meza 2,259 na viti 2,689 kwa shule za sekondari , wadau
baada ya kuona ukubwa wa tatizo wakaamua kuchangia kiasi hicho,”alisema.
Mbunge wa
jimbo hilo Mwalimu Marwa Ryoba aliyechangia madawati 100 yenye thamani y ash 12
mil,alisema shule nyingi zinakabiliwa na matatizo ya ukosefu wa madawati,hali
ambayo inachangia kushuka kwa taaluma na ufaulu.
“Ofisi yangu
imetoa imetoa madawati 100 kwa kuanzia na tutaendelea kuchangia ili tuhakikishe
watoto wetu hawakai chini,na kitakachofuata ni vyumba vya madarasa,baada ya
hapa tutawaunganisha wana Serengeti waioshio nje ya mkoa huu waweze kuchangia
maendeleo ya wilaya yao,”alisema.
Mhifadhi wa
Ujilani Mwema wa hifadhi ya Taifa ya Serengeti Nuhu Daniel alisema Tanapa
imetoa sh 154 mil kwa wilaya nane zinazopakana na hifadhi hiyo na kila moja
imepata zaidi ya sh 18 mil kwa ajili ya madawati,”pia tumetengeneza madawati 30
kwa ajili ya shule ya msingi Fort Ikoma,na tutaendelea kusaidia jamii
inayotuzunguka kama ilivyo sera yetu,”alisema.
Mwenyekiti
wa halmashauri hiyo Juma Porini alisema halmashauri yake imetenga sh 100
milioni kwa ajili ya kutengeneza madawati,hivyo mchango huo wa wadau utasaidia
kupunguza ukubwa wa tatizo na kuwataka wadau wanaowazunguka washirikiane kusukuma mbele maendeleo ya
wilaya hiyo.
Mkurugenzi
wa Kibo Safari’s Willy Chamburo ambaye
anaendesha biashara ya utalii maeneo mbalimbali ikiwemo Serengeti alichangia
madawati 50 yenye thamani ya Sh 6 milioni na kuwataka wafanyabiashara wa wilaya
hiyo kuhakikisha wanashimana ili kuwajengea mazingira mazuri ya maisha watoto
wao.
Baadhi ya
wadau mbalimbali waliochangia ni pamoja wawekeza wa sekta ya
utalii,wafugaji,wasanii,bodaboda,wakulima,Serengeti Media Centre,Ikona Wmas
,wafanyabiashara,Benki za Nmb,Crdb,Posta na watumishi wa idara mbalimbali za umma.
Wilaya hiyo
ina shule za msingi 110 za serikali zenye jumla ya wanafunzi 76302,sekondari 21
zenye wanafunzi 9359,inakabiliwa na upungufu wa madawati 14,594 kwa shule za
msingi na sekondari meza 2259 na viti 2,689.
Mwisho.
Igizo la kikundi cha Nyota Njema liliwakonga nyoyo wadau waliohudhuria kikao cha kuweka mikakati ya maendeleo ambacho kilizaa harambee ya zaidi ya sh 111 milioni.
Mnada wa ng'ombe ulifanyika kwa ajili ya kukusanya fedha za utengenezaji wa madawati
mijadala mbalimbali inaendelea nje ya Ukumbi
Mnada wa Dvd ulifanyika ili kukusanya fedha za madawati
Dc Maftah Ally akitoa taarifa ya makusanyo na nini kitaendelea baada ya hapo ili kuhakikisha wanakamilisha kazi ya madawati
0 comments:
Post a Comment