Saturday, May 7, 2016
Home »
» MKUU WA MKOA WA MARA AKIKAGUA BARABARA INAYOJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI MJINI MUGUMU
MKUU WA MKOA WA MARA AKIKAGUA BARABARA INAYOJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI MJINI MUGUMU
Mkuu wa Mkoa wa Mara Magesa Mulongo aliyekanyaga juu ya daraja wakiwa na wataalam ,madiwani na wadau mbalimbali wakiangalia moja ya daraja kwenye barabara ya kilometa tatu inayojengwa kwa kiwango cha lami na kampuni ya Samota Ltd kwa gharama ya sh 1.2 bilioni kutoka mfuko wa barabara,
Barabara hiyo ilitakiwa kukabidhiwa mei 6 mwaka huu kwa mjibu wa mkataba ,hata hivyo kazi hiyo haijakamilika,kutokana na kusua sua kwa kazi hiyo Mkuu wa Mkoa ameunda kikosi maalum cha uchunguzi ambacho kitatoa taarifa ndani ya wiki moja ili kubaini wanaochangia kukwama kwa mradi huo waweze kuchukuliwa hatua
Mhandisi wa wilaya ya Serengeti Sospeter Leonidas mwenye karatasi akitoa taarifa kwa mkuu wa Mkoa wa Mara juu ya utekelezaji wa ujenzi wa barabara ya lami
Wahandisi kutoka Tanrod na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wakiangalia BOQ ya mradi wa barabara
Ukaguzi unaendelea
Hapo wanaangalia mtaro ambao unadaiwa kujengwa kwa kutumia mawe chepechepe ambayo hupukutika yenyewe ikiwa ni kinyume cha mkataba
Ukaguzi wa daraja
Mjadala unaendelea kuhusiana na daraja hilo lilivyojengwa
0 comments:
Post a Comment