MAJI SUKARI YAWATESA WAKAZI WA MJI WA MUGUMU
SERENGETI MEDIA CENTRE
Wakazi wa Mji wa Mugumu wilayani hapa Mkoa wa Mara
wanakabiliwa na ukosefu wa maji safi kwa zaidi ya wiki mbili kufuatia mtambo wa
kusukuma maji kutoka bwawa la Manchira kuungua.
Wakati sukari ikiuzwa kati yash 3000-hadi 3500 kwa kilo na ikitolewa
Nchini Kenya kwa njia za panya,ndoo ya maji imepanda kutoka sh 100 kwa maji ya bomba hadi sh 500 kwa maji ya shimoni
na visima ,hali ambayo inazidisha makali ya maisha kwa wananchi na ni tishio la
ongezeko la magonjwa yanayosababishwa na maji..
Baadhi ya wakazi wa mji huo walisemalicha ya maji waliyokuwa
wanapata kutoka bwawa la Manchira kutokutibiwa lakini yalikuwa yanapatikana kwenye mabomba
kwa wakati wote na kwa gharama nafuu,ukilinganisha na hali ilivyo sasa ambapo
wengi wanalazimika kuamka alfajiri kwenda kutafuta kwenye visima vya watu.
Meneja wa Mamlaka ya Maji Mugumu Dickson Kasese akiongea na Serengeti
Media Centre kwa njia ya simu alidai kuwa mtambo wa kusukuma maji umeungua
kutokana na hitilafu ya umeme na kuwa zinatakiwa zaidi ya sh 180 mil za kununua
mwingine.
“Inahitajika Pampu mpya maana Control Panel,Cable ya
kuendesha motor zote zimekufa,tatizo hilo limebebwa na Mamlaka ya Maji Musoma
,na mtambo huo hapa nchini hakuna wameagiza nje ,itachukua zaidi ya wiki nne,tunatarajia
mwishoni mwa mwezi juni au mwanzoni mwa julai kama hatutapata njia nyingine ya dharura,”alisema.
Alisema kwa sasa yuko Dar es Salaam wizara ya Maji ili
kuwasilisha ombi la kupata mtambo mwingine utakaosaidia kutoa huduma kwa wananchi,hata
hivyo alisema maelezo yao yanadai kuwa hawana mpaka waagize nje na hautapatikana kwa muda mfupi kwa kuwa
mpaka watengenezewe kiwandani.
Consolatha John,Esther Magige wakazi wa mtaa wa NHC mjini
Mugumu walisema kuwa maji wanayouziwa kwa
sh 500 ni ya kwenye madimbwi ambayo yametuama wakati wa mvua,hivyo kama
tatizo hilo halitapata ufumbuzi wa haraka huenda kukaibuka magonjwa ya mlipuko
chanzo kikiwa maji.
Baadhi ya taasisi zilizokwishaanza onja adha ya ukosefu wa
maji ni pamoja na hospitali Teule ya
Nyerere,gereza mahabusu,Kituo cha Nyumba Salama ,Machinjio na wafanyabiashara wa nyumba za kulala
wageni,migahawa na hoteli ambazo zilitegemea maji ya bomba kutoka bwawa la
Manchira.
Hata hivyo baadhi ya wauza maji walisema kwa sasa wanapata
faida kubwa nakudai kama matengenezo yatachukua muda mrefu wanategemea bei ya
maji itapanda kwa kuwa hitaji litakuwa kubwa.
Mwisho.
Baadhi ya wakazi wa Mtaa Mwema mjini Mugumu wakichota maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali katika kisima cha Chakuburya,
Baadhi wa kazi wa mji wa Mugumu wakichota maji kwenye mtaro wa barabara eneo la Mkuu wa wilaya kwa ajii ya matumizi ya nyumbani,maji hayo ambayo si safi na salama.
0 comments:
Post a Comment