Fahari ya Serengeti

Monday, January 29, 2018

WAJITOKEZA KWA WINGI UZINDUZI WA WIKI YA SHERIA

 Viongozi mbalimbali wa wilaya wakiwa na watumishi wa Mahakama ya wilaya ya Serengeti kwenye maandamano ya Uzinduzi wa Wiki ya Sheria yenye Kauli mbiu ya ,MATUMIZI YA TEHAMA KATIKA UTOAJI HAKI KWA WAKATI NA KWA KUZINGATIA MAADILI.
 Baadhi ya watoto wa kike waliokimbia kukeketwa wakipaza sauti juu ya utendaji wa Haki kwa wakati kunavyosaidia ustawi wa Jamii.
 Wanapaza sauti
 Maandamano yanaendelea kama ilivyopangwa
 Wanafunzi hawakubaki nyuma
 Wanasonga mbele
 Wanakatisha mjini wakipaza sauti
 Ujumbe unatolewa kwa njia za nyimbo na mabango
 Mwalimu anaelekeza
 Wanasonga kwa kasi

 Wanaendelea
 Makamanda hawakubaki nyuma
Katibu tawala wilaya Cosmas Qamara akitoa nasaha kwa wadau mbalimbali

UZINDUZI WA WIKI YA SHERIA WAWAKUTANISHA WADAU MBALIMBALI SERENGETI

 Katibu Tawala wilaya ya Serengeti Cosmas Qamara kulia akiongoza maandamano ya ufunguzi wa wiki ya sheria ambayo yameshirikisha wadau mbalimbali wilayani hapa.
 Wanafunzi wakipaza sauti kupeleka ujumbe kwa wadau mbalimbali wakati wa maandamano ya uzinduzi wa wiki ya sheria wilaya ya Serengeti
 Wanasonga huku wakiwa wamebeba ujumbe ambao ni kauli mbiu ya wiki ya Sheria,MATUMIZI YA TEHAMAKATIKA UTOAJI WA HAKI.

Asiye na mwana alibeba mbeleko mwenye mwana akabeba mwana

Friday, January 26, 2018

UCHENJUAJI WA DHAHABU KARIBU NA CHANZO CHA MAJI KWAWATIA HOFU WANANCHI

 Wakazi wa kijiji cha Merenga kata ya Nyansurura wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara wameomba serikali ichukue hatua za haraka kuwanusuru kufuatia mtu mmoja kuanzisha kazi ya kuchenjua dhahabu kwa kutumia kemikali aina ya Zebaki karibu na chanzo cha Maji wanachotumia kwa ajili ya maji ya kunywa.

Kazi hiyo ambayo uongozi wa kijiji unadai kuwa inafanywa bila kibali cha Tathimini ya Mazingira inadaiwa kuendelea kwa kasi na maji wanayotumia yakidaiwa kutiririka na kurudi kwenye lambo wanalotegemea kama chanzo chao cha maji ya kunywa,kupikia,kufua na kunywesha mifugo.

Idara ya Mazingira halmashauri ya wilaya ya Serengeti imekana kuwapa kibali wahusika kwa madai kuwa waliombwa kuandaa mpango wa athari ya Mazingira lakini hawakufanya hivyo,hata hivyo wameahidi kuchukua hatua haraka.
 Baadhi ya akina mama wanaofanya kibarua cha kusomba maji na kuchenjua dhahabu
 Pamoja na tishio la kemikali ya Zebaki,pia imebainika kuwa hawana choo na watu wanajisaidia vichakani na wakati wa mvua uchafu wote hutiririka kwenda lamboni.

wanakwenda kufanya kibarua

Monday, January 22, 2018

ASKOFU AWAONGOZA MAPADRI KUADHIMISHA MISA YA KUTABARUKU ALTARE

 Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Musoma Michael Msonganzila akiwaongoza mapadri wa jimbo hilo katika mageuzo ya Ekaristi Takatifu wakati wa Misa ya Kuabaruku altare ya Kanisa Katoliki Parokia ya Issenye na kuadhimisha Jubilei ya Miaka 10 toka amepata uaskofu.
 Mapadri wakitoa komnio kwa waumini

 Pongezi za kutimiza miaka 10 ya uaskofu zilizoambatana na zawadi zilitolewa
 Mapadri wanampongeza baba askofu kwa kutimiza miaka 10 ya uaskofu toka amechaguliwa.
 Mwenyekiti wa baraza la Walei Jimbo Katoliki Musoma Raymondi Nyamasagi na Makamu wake nao walimpongeza Baba askofu ,Masista na Paroko Kenedy Gurusha na kutoa zawadi za Ng'ombe na Kondoo
 Nasaha zilitolewa
 Picha ya Pamoja ilipigwa





ASKOFU ATABARUKU ALTARE YA KANISA KATOLIKI ISSENYE

 Baba Askofu wa Jimbo Katoliki Musoma Michael Msonganzila akitabaruku altare ya kanisa Katoliki Parokia ya Issenye ikiashiria kuanza kutumika kwa ajili ya misa takatifu,kazi hiyo imekwenda sambamba na kuadhimisha Jubilei ya Miaka 10 toka amepata uaskofu.
 Ibada inaendelea ya kutabaruku



Sunday, January 21, 2018

MBUNGE AWATAKA WAKAZI WA MAKUNDUSI KUWADHIBITI WANAOKWAMISHA MAENDELEO

 Mbunge wa Jimbo la Serengeti Mkoa wa Mara Marwa Ryoba amekemea tabia za baadhi ya wakazi wa kijiji cha Makundusi wanaondesha kampeini za kukwamisha maendeleo ya kijiji ,kuwa hao hawatakiwi kuwavumilia kwa kuwa wanaangalia maslahi yao badala ya jamii.

Katika mkutano wake wa hadhara kijijini hapo amaewataka watu wanaondesha kampeini za kupinga maendeleo,mikutano isifanyike kuwa muda wa siasa wasubiri mwaka kesho na mwaka 2020 kwa kuwa sasa ni kipindi cha kufanya maendeleo kwa maslahi ya kijiji,wilaya na Taifa.

"Tumieni mikutano yenu kuhoji mambo yanayohitaji ufafanuzi,si kufanya kampeini za kuvuruga mikutano ili wananchi wasiambiwe ukweli,harafu mnatoka na tuhuma kwa viongozi ambazo wananchi hawazijui,acheni vitendo hivyo kwa kuwa havilengi kuwasaidia wananchi bali kuwakwamisha kimaendeleo,hata kama mnataka madaraka wananchi ndiyo waamzi,"amesema.

Amewataka viongozi kuendelea kushikamana na wananchi kwa ajili ya maendeleo,na kuwapongeza kutokana na kutekeleza miradi mikubwa na mizuri kwa fedha za kijiji.
 Anasisitiza jambo
 Mnanielewa?


Wanafuatilia hotuba ya Mbunge

WAKAZI WA MAKUNDUSI WARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

 Mwenyekiti wa serikali ya Kijiji cha Makundusi kata ya Natta wilaya ya Serengeti Juma Porini akitoa ufafanuzi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo na fedha zilizotumika wakati wa mkutano wa hadhara wa kijiji,wananchi wameridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo na hakuna ubadhirifu uliofanyika.

Wananchi wamekemea watu wanaotumika kisiasa kuchafuana na kuwataka wawe na hoja zenye uthibitisho na kuwataka wasubiri muda wa Kampeini ndipo waendeshe siasa zao kwa kuwa sasa ni utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Mwenyekiti huyo amesema yeye si mweka sahihi katika akaunti ya kijiji hivyo hana uwezo wa kuchukua fedha na kuzitumia kama baadhi ya watu walivyodai,"fedha za kijiji zinatolewa kwa utaratibu kuanzia kijijini ,kata na muidhinishaji wa mwisho ni Mkurugenzi Mtendaji,na mwenyekiti hana sahihi katika zoezi hilo,wapuuzeni wanapiga siasa zisizo na tija na tunapoitisha mkutano wapate taaraifa hawafiki na wengine wanaendesha kampeini watu wasihudhurie,"amasema Porini

 Wakazi wa kijiji cha Makundusi wakiwa kwenye mkutano wa hadhara.

 Wanafuatilia mkutano wa hadhara
 Anachangia hoja