Fahari ya Serengeti

Sunday, January 21, 2018

MBUNGE AWATAKA WAKAZI WA MAKUNDUSI KUWADHIBITI WANAOKWAMISHA MAENDELEO

 Mbunge wa Jimbo la Serengeti Mkoa wa Mara Marwa Ryoba amekemea tabia za baadhi ya wakazi wa kijiji cha Makundusi wanaondesha kampeini za kukwamisha maendeleo ya kijiji ,kuwa hao hawatakiwi kuwavumilia kwa kuwa wanaangalia maslahi yao badala ya jamii.

Katika mkutano wake wa hadhara kijijini hapo amaewataka watu wanaondesha kampeini za kupinga maendeleo,mikutano isifanyike kuwa muda wa siasa wasubiri mwaka kesho na mwaka 2020 kwa kuwa sasa ni kipindi cha kufanya maendeleo kwa maslahi ya kijiji,wilaya na Taifa.

"Tumieni mikutano yenu kuhoji mambo yanayohitaji ufafanuzi,si kufanya kampeini za kuvuruga mikutano ili wananchi wasiambiwe ukweli,harafu mnatoka na tuhuma kwa viongozi ambazo wananchi hawazijui,acheni vitendo hivyo kwa kuwa havilengi kuwasaidia wananchi bali kuwakwamisha kimaendeleo,hata kama mnataka madaraka wananchi ndiyo waamzi,"amesema.

Amewataka viongozi kuendelea kushikamana na wananchi kwa ajili ya maendeleo,na kuwapongeza kutokana na kutekeleza miradi mikubwa na mizuri kwa fedha za kijiji.
 Anasisitiza jambo
 Mnanielewa?


Wanafuatilia hotuba ya Mbunge

0 comments:

Post a Comment