Fahari ya Serengeti

Sunday, January 21, 2018

WAKAZI WA MAKUNDUSI WARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

 Mwenyekiti wa serikali ya Kijiji cha Makundusi kata ya Natta wilaya ya Serengeti Juma Porini akitoa ufafanuzi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo na fedha zilizotumika wakati wa mkutano wa hadhara wa kijiji,wananchi wameridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo na hakuna ubadhirifu uliofanyika.

Wananchi wamekemea watu wanaotumika kisiasa kuchafuana na kuwataka wawe na hoja zenye uthibitisho na kuwataka wasubiri muda wa Kampeini ndipo waendeshe siasa zao kwa kuwa sasa ni utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Mwenyekiti huyo amesema yeye si mweka sahihi katika akaunti ya kijiji hivyo hana uwezo wa kuchukua fedha na kuzitumia kama baadhi ya watu walivyodai,"fedha za kijiji zinatolewa kwa utaratibu kuanzia kijijini ,kata na muidhinishaji wa mwisho ni Mkurugenzi Mtendaji,na mwenyekiti hana sahihi katika zoezi hilo,wapuuzeni wanapiga siasa zisizo na tija na tunapoitisha mkutano wapate taaraifa hawafiki na wengine wanaendesha kampeini watu wasihudhurie,"amasema Porini

 Wakazi wa kijiji cha Makundusi wakiwa kwenye mkutano wa hadhara.

 Wanafuatilia mkutano wa hadhara
 Anachangia hoja


1 comment:

  1. Acheni siasa nyakitono nawapenda saana hongereni kwa maendeleo acheni siasa na kuniibia wenyewe
    hizo mali ni zenu na vizazi vyenu hamna kiongozi ataenda nazo kwake

    ReplyDelete