Fahari ya Serengeti

Friday, January 26, 2018

UCHENJUAJI WA DHAHABU KARIBU NA CHANZO CHA MAJI KWAWATIA HOFU WANANCHI

 Wakazi wa kijiji cha Merenga kata ya Nyansurura wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara wameomba serikali ichukue hatua za haraka kuwanusuru kufuatia mtu mmoja kuanzisha kazi ya kuchenjua dhahabu kwa kutumia kemikali aina ya Zebaki karibu na chanzo cha Maji wanachotumia kwa ajili ya maji ya kunywa.

Kazi hiyo ambayo uongozi wa kijiji unadai kuwa inafanywa bila kibali cha Tathimini ya Mazingira inadaiwa kuendelea kwa kasi na maji wanayotumia yakidaiwa kutiririka na kurudi kwenye lambo wanalotegemea kama chanzo chao cha maji ya kunywa,kupikia,kufua na kunywesha mifugo.

Idara ya Mazingira halmashauri ya wilaya ya Serengeti imekana kuwapa kibali wahusika kwa madai kuwa waliombwa kuandaa mpango wa athari ya Mazingira lakini hawakufanya hivyo,hata hivyo wameahidi kuchukua hatua haraka.
 Baadhi ya akina mama wanaofanya kibarua cha kusomba maji na kuchenjua dhahabu
 Pamoja na tishio la kemikali ya Zebaki,pia imebainika kuwa hawana choo na watu wanajisaidia vichakani na wakati wa mvua uchafu wote hutiririka kwenda lamboni.

wanakwenda kufanya kibarua

0 comments:

Post a Comment