Fahari ya Serengeti

Thursday, July 27, 2017

TAKUKURU YAMPANDISHA KIZIMBANI MKURUGENZI WA MUWASA KWA KUGHUSHI NYARAKA

SERENGETI MEDIA CENTRE.

Mara .Mkurugenzi wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Musoma  Hawaju Said Gantala (42)amefikishwa katika mahakama ya wilaya Musoma kwa Makosa 15 ya kughushi nyaraka na kujipatia sh 63,400,000 kinyume cha sheria.
Mbele ya hakimu wa mahakama hiyo  Karimu Mushi ,wakili wa Takukuru Mkoa wa Mara Moses Malewo katika kesi ya Jinai namba 176/2017 aliliambia mahakama hiyo Kuwa Mshitakiwa anakabiliwa na Makosa hayo ya kughushi kujipatia fedha kwanjia  ya udanganyifu  na kuwasilisha nyaraka za kupotosha katika benki zaCrdb na NBC matawi ya Musoma.
Alisema kwa kosa la kwanza hadi la tano Mshitakiwa anakabiliwa na Makosa yakughushi nyaraka za kuingiziwa mshahara (salary slip) za Septemba hadi desemba 2014 ,kughushi nyaraka za kuingiziwa mshahara wa juni,Julai na Agosti 2016 kwa kuonyesha kwamba ni nyaraka halali kutoka MUWASA huku akifahamu Kuwa si kweli.
Alibainisha kuwa katika kosa la sita Gantala ili hali akijua kuwa si kweli aliwasilisha nyaraka za kuingiziwa fedha benki ya Crdb Tawi la Musoma ambazo zilikuwa zikionyesha kuwa katika mwezi septemba na desemba 2014 mshahara wake ulikuwa sh 2,767,549 na kujipatia mkopo wa sh 30 mil kinyume cha sheria.
Malewo aliiambia mahakama kuwa kosa la saba mshitakiwa  katika kipindi cha juni,julai na agosti 2016 alijipatia  mkopo wa sh 34,400,000 kutoka Benki ya Nbc Tawi la Musoma kwa kutumia nyaraka za kuingiziwa mshahara(salary slip) za uongo zikionyesha kwamba mshahara wake ni sh 2,636,179.82 kinyume cha sheria.
Kwa kosa la 8 hadi 13 Gantala akijua ni kosa aliwasilisha nyaraka zauongo za  kuingiziwa mshahara wa mtumishi katika benki ya Crdb na Nbc Matawi ya Musoma akidanganya kuwa ni halali kutoka Muwasa na kujipatia jumla ya  sh 63,400,000 toka benki hizo.
Kwa kosa la 14 Wakili huyo wa Takukuru alisema Gantala alimlaghai Mkuu wa Idara ya Utawala MUWASA Brian D.Moshi kuweka saini hati za kuingiziwa mshahara wa Mtumishi (Salary Slip)kwa miezi ya juni,julai na agosti mwaka 2016 ili zionekane ni hati toka Muwasa.
Alifafanua kuwa alifanya hivyo wakati akijua kuwa si nyaraka halali na zililenga kuzipotosha taasisi hizo za fedha kinyume cha sheria.
Katika shitaka la 15 mshitakiwa alimlaghai Issaya Maswi Nyaibo mkuu wa idara ya fedha MUWASA na kutia saini hati za kuingizwa mshahara wa mtumishi (Salary Slip)za kughushi kwa miezi ya septemba,oktoba na novemba 2014 ili zionekane ni hati halali toka Muwasa wakati akijua ni makosa.
Mshitakiwa amekana mashitaka hayo na yuko nje kwa dhamana ya wadhamini wawili kila mmoja kwa kuwa na hati ya mali isiyohamishika yenye thamani kama kiasi hicho na kesi hiyo itatajwa agosti 22 mwaka huu.

Mwisho.

Wednesday, July 26, 2017

KILIO CHA TOZO ZA SINGLE ENTRY CHAWAKUTANISHA WADAU

 Katibu wa Ikona Wma iliyoko wilayani Serengeti Yusuph Manyanda akisoma changamoto zinazotokana na Tozo ya Single Entry kwa wawekezaji walioko nje ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti ikiwemo kupungua kwa wageni,baadhi ya kambi kufungwa ,vijana kukosa ajira,mapato ya Wma kupungua ,na wananchi kuchukia uhifadhi,hata hivyo katika kikao hicho kilichohudhuriwa na Mkurugenzi wa Tanapa Allan Kijazi wamekubaliana kuunda timu ili kuchambua changamoto hizo na nyingine lengo likiwa ni kubaini ukweli kwa takwimu,kabla ya tozo hali ilikuwaje na baada ya Tozo na nini kifanyike.
 Dc Serengeti Nurdin Babu akielezea umuhimu wa wadau kukaa pamoja ili kuja na mkakati wa pampja mbao utaisaidia serikali kuchukua hatua stahiki kuhusiana na tozo hizo.
 Baadhi ya wajumbe wa Ikona Wma  wakifuatilia mjadala
 Wanafuatilia
 wako makini
 Mbunge wa Jimbo la Serengeti Marwa Ryoba akiwa na viongozi wengine wakifuatilia mjadala huo
 Makabrasha yanapitiwa kwa makini
 Katibu anawasilisha changamoto

 Mbunge anafafanua alivyofuatilia kwenye kamati ya Bunge ya Maliasili na kuwasilisha hoja bungeni kuhusiana na tatizo la tozo hiyo kwa Wma ya Ikona
 Mkurugenzi wa Tanapa Allan Kijazi anapokea taarifa toka kwa katibu wa Ikona Wma Yusuph Manyanda
 Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri Ikona Wma Sospeter Nyigoti akitoa ufafanuzi wa athari ya tozo hiyo
 wanapitia kipengele kwa kipengele

 Palangyo kwa niaba ya wawekezaji akieleza athari wanazopata kutokana na tozo hiyo
Mkurugenzi wa Tanapa Allan Kijazi akitoa ufafanuzi wa tozo hiyo ilivyo kisheria na inatakiwa kuondolewa kwa misingi ya kisheria kama itaonekana ina athari,amesema timu ya pande zote itakuja na majibu muafaka ,hata hivyo amesema taarifa iliyowasilishwa haitoi picha ya tatizo kwa kuwa hakuna takwimu zinazoonyesha mapato yamepumgua kutoka ngapi hadi ngapi

Monday, July 24, 2017

ZIARA YA KAMATI YA FEDHA MIPANGO NA UCHUMI YABAINI MAMBO MENGI

 Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti Juma Porini wa pili kulia akiwa na wajumbe wa kamati ya Fedha Mipango na Uchumi wakati wakikagua miradi ya maendeleo .
 Afisa Tabibu wa zahanati ya Rung'abure Johstone Bushanya akielezea sababu za waganga kutokuwepo kazini bila ruksa.
 Ukaguzi unaendelea


Mwenyekiti Juma Porini akikagua darasa la shule ya Msingi Nyansurumunti



 Umejibu vemaa


CRDB BANK YAAHIDI KUUNGANA NA WADAU KUTANGAZA UTALII WA NDANI

 Meneja wa Crdb Bank Tawi la Mugumu wilaya ya Serengeti Melkoir Mapunda akimwelezea Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu jinsi Bank hiyo ilivyojipanga kusaidiana na wadau mbalimbali kutangaza utalii wa ndani ili kusaidia jamii kutumia fursa hiyo kwa ajili ya kujipatia mapato yao.
Ili kuhakikisha fursa hiyo inanufaisha jamii ,benki hiyo ni miongoni mwa wadau waliochangia maonesho ya Serengeti Festival Culture yaliyofanyika kwa siku tatu mjini Mugumu,
Mapunda amesema jitihada kubwa zinatakiwa kuelekezwa kwenye utalii wa utamaduni ili kusaidia kunyanyua uchumi wa jamii na Taifa kwa haraka.



Wednesday, July 19, 2017

MAONESHO YA SABA YA UTALII WA KITAMADUNI YAFUNGULIWA SERENGETI

 Mmoja wa washiriki katika maonesho ya Serengeti Cultural Festival kutoka Mbeya akiwa na bidhaa yake ya madawa ya asili,Mkuu wa wilaya Nurdin Babu kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk Charles Mlingwa amefungua rasmi maonesho hayo ya siku tatu.
 Wajasiriamali wa bidhaa mbalimbali walikuwepo,hilo ni Banda la Serengeti Group
 Msanii kutoka jijini Mwanza akisuka zulia kutumia nyuzi.



 Stephen Muhegete mmoja wa wakulima wa mboga mboga anazolima akiwa katika banda la maonesho kwa ajili ya kutoa elimu

 Burudani zinaendelea
 Kikundi cha ngoma ya Wamasai toka Robanda wakiingia uwanjani kwa ajili ya kutoa burudani
 Burudani zinaendelea
 Msanii kutoka Butiama
 Dc Serengeti akikagua mabanda
 Mjasriamali kutoka Mwanza akimpa Dc Maelezo ya bidhaa yake

 Dawa mbalimbali za asili kutoka kwa Dk Hoza kutoka Mbeya


 wanaangalia bidhaa aina mbalimbali
 Mapambo,shanga na bangili zilikuwepo



 Kikundi cha maua Mugumu
 Dc akisaini kwenye kitabu cha Serengeti Group



 Wanapata msosi



 Wana chuo cha Utalii Srengeti walikuwepo
 Mambo ya Setco
 Setco wakonga nyoyo za washiriki kwa maandalizi ya bidhaa zao ikiwemo keki,mikate na chakula


 Ulipo Tupo,CRDB Benki walikuwa mstari wa mbele

 NMB BENKI nao wameshiriki kwa nguvu zote


 Banda la Takukuru Serengeti

 NSSF MARA WAMESHIRIKI




 Banda la Maliasili na Utalii lililojumuisha bodi ya Utali na Tanapa


 Banda la Air Tanzania