Fahari ya Serengeti

Thursday, July 13, 2017

TPB BANK YAPIGA JEKI SHULE YA MSINGI KETEMBERE SERENGETI



Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk Charles Mlingwa akipokea na kuzindua Mradi wa byumba vya Madarasa viwili,ofisi mbili za walimu,madawati 30,meza mbili za walimu na choo cha matundu 8 kwa gharama ya zaidi ya sh 71 mil,iliyojengwa na TPB BANK kwa ajili ya shule ya Msingi Ketembere wilayani Serengeti,kushoto ni Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Robert Bashite.


Madarasa mawili na ofisi mbili za walimu shule ya Msingi Ketembere wilaya ya Serengeti yaliyojengwa na TPB BANK


 Burudani zilikonga nyoyo za watu.
 Mkuu wa Mkoa akisisitiza jambo kwa jamii kutokana na msaada huo ambao umesaidia kupunguza ukubwa wa tatizo la madarasa linaliokabili shule hiyo yenye watoto 712 ina vyumba nane vya madarasa hali ambayo inawafanya watoto kurundikana katika chumba kimoja na kuathiri mfumo mzima wa kujifunza na kujifunzia.

 Mkurugenzi Mtendaji wa TPB  Bank Sabasaba Mashingi akielezea kilichowasukuma kujenga vyumba viwili vya madarasa,vyumba viwili vya Ofisi,madawati 30,meza mbili za walimu na choo cha matundu manane shule ya Msingi Ketembere wilayani Serengeti kwa gharama ya zaidi ya sh 71 mil,ni baada ya timu ya ufuatiliaji kujiridhisha na hali mbaya ya shule ilianza mwaka 1976 .
Amesema TPB BANK kupitia bajeti yao ya zaidi ya sh 150 mil wanayotenga kwa ajili ya kusaidia miradi ya maendeleo waliamua kusaidia,lengo ni kuwawezesha watoto kupata elimu katika mazingira mazuri.
 Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk Charles Mlingwa akijadili jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa TPB BANK Sabasaba Mashingi ,katikati ni Mbunge wa jimbo la Serengeti Marwa Ryoba.

 Picha ya viongozi mbalimbali mbele ya jengo wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mara dk Mlingwa.

 Burudani mbalimbali zilikuwepo,hiyo ni ngoma maarufu ya Gorona ya jamii ya Watatoga wilayani Serengeti.
 Baadhi ya maafisa wa TPB BANK wakifuatilia matukio mbalimbali.
 Kila aliyeguswa hakujizuia bali aliweza kutoa kitu kwa wacheza ngoma.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TPB BANK Sabasaba Mashingi akicheza ngoma ya asili ya Watatoga ambayo ndiyo asili yake,

 Anapongezwa na mmoja wa wazee kwa jinsi alivyoweza kusakata ngoma yao ya asili,wahenga walisema msahau kwao ni mtumwa.
 Uzinduzi ukafanyika.



0 comments:

Post a Comment