Fahari ya Serengeti

Wednesday, July 26, 2017

KILIO CHA TOZO ZA SINGLE ENTRY CHAWAKUTANISHA WADAU

 Katibu wa Ikona Wma iliyoko wilayani Serengeti Yusuph Manyanda akisoma changamoto zinazotokana na Tozo ya Single Entry kwa wawekezaji walioko nje ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti ikiwemo kupungua kwa wageni,baadhi ya kambi kufungwa ,vijana kukosa ajira,mapato ya Wma kupungua ,na wananchi kuchukia uhifadhi,hata hivyo katika kikao hicho kilichohudhuriwa na Mkurugenzi wa Tanapa Allan Kijazi wamekubaliana kuunda timu ili kuchambua changamoto hizo na nyingine lengo likiwa ni kubaini ukweli kwa takwimu,kabla ya tozo hali ilikuwaje na baada ya Tozo na nini kifanyike.
 Dc Serengeti Nurdin Babu akielezea umuhimu wa wadau kukaa pamoja ili kuja na mkakati wa pampja mbao utaisaidia serikali kuchukua hatua stahiki kuhusiana na tozo hizo.
 Baadhi ya wajumbe wa Ikona Wma  wakifuatilia mjadala
 Wanafuatilia
 wako makini
 Mbunge wa Jimbo la Serengeti Marwa Ryoba akiwa na viongozi wengine wakifuatilia mjadala huo
 Makabrasha yanapitiwa kwa makini
 Katibu anawasilisha changamoto

 Mbunge anafafanua alivyofuatilia kwenye kamati ya Bunge ya Maliasili na kuwasilisha hoja bungeni kuhusiana na tatizo la tozo hiyo kwa Wma ya Ikona
 Mkurugenzi wa Tanapa Allan Kijazi anapokea taarifa toka kwa katibu wa Ikona Wma Yusuph Manyanda
 Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri Ikona Wma Sospeter Nyigoti akitoa ufafanuzi wa athari ya tozo hiyo
 wanapitia kipengele kwa kipengele

 Palangyo kwa niaba ya wawekezaji akieleza athari wanazopata kutokana na tozo hiyo
Mkurugenzi wa Tanapa Allan Kijazi akitoa ufafanuzi wa tozo hiyo ilivyo kisheria na inatakiwa kuondolewa kwa misingi ya kisheria kama itaonekana ina athari,amesema timu ya pande zote itakuja na majibu muafaka ,hata hivyo amesema taarifa iliyowasilishwa haitoi picha ya tatizo kwa kuwa hakuna takwimu zinazoonyesha mapato yamepumgua kutoka ngapi hadi ngapi

0 comments:

Post a Comment