Fahari ya Serengeti

Friday, August 19, 2016

Mratibu wa mradi wa pamoja Tuwalee wilaya ya Serengeti Christopher Genya kulia akimkabidhi nyaraka za mradi huo ambao umemaliza muda wake afisa maendeleo ya Jamii wilaya Sunday Wambura katikati ni afisa ustawi wa jamii Faustine Matesi


 ZAIDI YA SH 308 MIL.ZANUFAISHA VIKUNDI VYA WATOTO WA MAZINGIRA HATARISHI,
Serengeti Media Centre.
Zaidi ya sh 308 milioni zimekopeshwa kwa vikundi 96 vya Watoto waishio katika Mazingira Hatarishi kupitia Mradi wa Pamoja Tuwalee wilayani Serengeti Mkoa wa Mara kwa kipindi cha mwaka 2011hadi 2016.
Mradi wa Pamoja Tuwalee ambao umefikia ukomo ulikuwa unaendeshwa na Shirika la Pact Tanzania kwa kushirikiana na asasi ya BAK-AIDS kwa ufadhili wa USAID/PEPFAR katika kata 17 kati ya 30 za wilayani hapa,na kuwezesha akina mama wengi kujihusisha na shughuli za bustani za mboga mboga ambazo zimewawezesha kuweka akiba.
Mratibu wa Mradi wa BAK-AID wilaya ya Serengeti Christopher Genya kwenye kikao cha wadau wa maendeleo wilaya wakati wa kukabidhi shughuli za mradi huo kwa  halmashauri alisema,vikundi hivyo vina akiba y ash 331,162,260,na wanaendesha biashara mbalimbali 1473 katika maeneo yao.
“Kupitia mradi huu watoto 4517 kati ya 8,046 wanalelewa na walezi walio katika vikundi,na kaya 1,839 zimenufaika na mradi huo na wameweza kuboresha makazi yao,wengine wamenunua mifugo,na waliokuwa wanakula mlo mmoja sasa wanakula milo mitatu,na mafanikio makubwa ni kwamba wanajisimamia wenyewe,”alisema.
Hata hivyo alisema katika utekelezaji wa mradi huo walikabiliana na changamoto za baadhi ya kamati za watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi kutokuwasaidia watoto,ikiwemo kutokushirikishwa katika vikao vya serikali za vijiji na kata.
Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya ambaye pia ni afisa maendeleo ya jamii Sunday Wambura aliwataka wadau wa maendeleo kuhakikisha katika shughuli zao wanaweka mipango ya kuwasaidia watoto wa mazingira hatarishi,kwa kuwa hilo ni jukumu la kila mmoja.
Mapema afisa mradi huo Eza Yusuph alisema lengo kuu lilikuwa kuimarisha mifumo iliyopo ya jamii na familia zao,kuongeza rasilimali za ndani na nje katika kufikia mahitaji ya watoto na  mfumo wa ustawi wa familia baada ya kukosekana kwa msaada toka nje.
Mwisho.












VIKUNDI VYA VIJANA NA WANAWAKE VYAPEWA MAMILIONI YA FEDHA

Serengeti Media Centre.
Halmashauri ya  wilayani hapa Mkoa wa Mara imejipanga kuhakikisha fursa zinazowazunguka hasa za utalii na uhifadhi zinachangia kuchochea kukua kwa uchumi wa jamii na wilaya hiyo.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Juma Porini akizindua awamu ya pili ya utoaji wa mikopo kwa wanawake na vijana kupitia asilimia tano ya makusanyo ya ndani jana ,alisema lengo lao ni kuona fursa hizo zinawanufaisha wajasiriamali wakubwa kwa wadogo wakiwemo wakulima wanaozalisha mazao yao na kukosa soko badala yake wanaambulia madhara yanayosababishwa na uhifadhi na utalii.
Alisema jumla ya sh 128 milioni zimetolewa kwa vikundi 55  vya wanawake vikiwa 33  na vijana 22 toka machi mwaka huu ikiwa ni  bajeti ya mwaka wa fedha 2015/16,lakini kumekuwa na tatizo la soko hasa kwenye mahoteli na kambi za kitalii zilizomo ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti,ili kuhakikisha wanafungua mahusiano mazuri na jamii inayowazunguka alisema wamepanga kutembelea fursa hizo ili wajadiliane changamoto zilizopo na namna ya utatuzi.
“Wakati tunahangaika kufungua milango ya fursa zinazotuzunguka ,ni vema nanyi kujitahidi kuzalisha bidhaa zenye ubora ili kuendana na soko,na pia mikopo hii ingawa ni kidogo  maana tunatoa sh 2 milioni kwa kikundi ziweze kusaidia kuleta tija kiuchumi kwa kila anayekopa,”alisema.
Alisema awali vikundi vingi vilivyokuwa vikinufaika na mikopo vilikuwa vya mjini,lakini kwa awamu ya uongozi wao waliazimia maeneo yote wanufaike na katika awamu ya pili ya mikopo kwa wanawake mjini wamepata vikundi viwili na vijijini 10 .
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Seif Hamsini alisema tatizo la wananchi kutonufaika na fursa za utalii zinazowazunguka ni la kitaifa na kuwa wanajitahidi kuondoa mazingira hayo,huku akiwasihi wanufaika na mikopo kama wanataka kushika soko la mahoteli ya kitalii waepuke kuzalisha mazao yao kwa kutumia kemikali za viwandani.
“Lazima kufanyike na mabadiliko ya uzalishaji ,wenzetu wa Uganda kwa nchi za Afrika Mashariki wamefanikiwa kushika soko hilo kwa kuwa wanazalisha mazao yao bila kutumia kemikali za viwandani ,nanyi pia tumieni njia za asili ili kulinda ubora wa matunda na mboga mboga mnazozalisha ili kupanua soko,”alisema.
Hata hivyo alikiri kuwa kiwango kinachotolewa ni kidogo cha sh 2 milioni ambazo ziko chini ya dola 1000 na kuwa watajitahidi kuona namna ya kuboresha mikopo,hata hivyo serikali kuu kutokutoa ruzuku ya maendeleo kwa bajeti ya mwaka 2015 ilifaya halmashauri itumie fedha za ndani kutekeleza miradi na kukopesha makundi hayo.
Afisa vijana wilaya Isack Mwankusye alisema watafanya ufuatiliaji kwa wanufaika wote kwa kuwa baadhi wamekuwa wakipata mikopo wanaelekeza kwenye shughuli ambazo hawakuombea.
Naye afisa maendeleo ya Jamii Hidaya Mkaruka aliwataka wanawake kuhakikisha wanarejesha kwa wakati kwa kuwa wasipofanya hivyo wanaiingiza halmashauri kwenye gharama za kuwafuatilia na pia kukwamisha wengine kukopa.
Mmoja wa wanufaika Mwita Chacha toka Kebanchabancha alishauri halmashauri ifikie hatua ya kukopesha mtu mmoja mmoja hasa baada ya kujiridhisha na kazi zake kwa kuwa kwenye vikundi watu wengi hawana mtizamo wa aina moja na ndiyo maana vinashindwa kupiga hatua za kimaendeleo.
Mwisho.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti Juma Porini akitoa nasaha kwa wanachama wa vikundi vya vijana na wanawake ambao wamepata mkopo wa fedha kupitia asilimia tano ya makusanyo ya ndani bajeti ya mwaka 2015/16 jumla ya sh 128 mil zimetolewa toka machi hadi sasa





Wednesday, August 10, 2016

MATUKIO YA SIKU YA FAINALI YA UMOJA CUP

Ng'ombe aliyetolewa kwa bingwa wa mashindano ya mpira ligi ya Umoja Cup akiwa amezungukwa na wachezaji na mashabiki mbalimbali wa Mageta Fc baada ya kuifunga Seronga Fc bao 1-0 katika Uwanja wa Sokoine Mjini Mugumu Serengeti ambayo iliandaliwa na Serengeti Media Centre,Magoiga na Mageta.Pia timu hiyo ilipata mpira na ilipata sh 40000 na cheti kama timu bora na mfungaji bora alitoka timu hiyo akajipatia sh 50,000.

MABINGWA WA UMOJA CUP MAGETA SPORT WAKIWA KATIKA UBORA WAO
TIMU ya Seronga Fc washindi wa pili Umoja Cup ambao walipata mbuzi na mpira mmoja wakiwa kwenye ubora wao kabla ya kuanza mchezo.
Waamzi wakiwa kwenye eneo lao wakifuatilia mchezo

Mashabiki wakiwa nje ya kamba wakifuatilia mpambano mkali kati ya Mageta Sports na Seronga Fc
Timu ya Polisi Fc waliambulia nafasi ya nne na kupata mpira mmoja.




Seronga fc wakipasha kabla ya kuingia uwanjani hata hivyo waliambulia kipigo kutoka kwa mahasimu wao Mageta Spots.
Mbunge wa jimbo la Serengeti Marwa Ryoba katikati mwenye gwanda la Chadema akifuatilia mchezo kulia ni katibu tawala wa wilaya Cosmas Qamara
Timu ya Mageta Fc

Ukaguzi mbunge akikagua timu ya Mageta Fc
Waamzi













Nasaha mbalimbali zikitolewa





















Mashindano ya kukimbia





Bingwa wa mbio mita 10000 Jumanne Ndege akiwa anapasha baada ya kumaliza mbio hizo kwa dkk 40 akiwa na mkuu wa shule ya sekondari Serengeti.