Fahari ya Serengeti

Tuesday, August 2, 2016

UMOJA CUP YAINGIA ROBO FAINALI KUANZIA AGOSTI 3 MWAKA HUU

 Dc Serengeti Nurdin Babu akiwaasa wachezaji kutumia furasa hiyo kucheza kwa amani kwa kuwa kupitia Umoja Cup wengine wanaweza kupata fursa ya kwenda kucheza maeneo mengine,na kuahidi kuwa wilaya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali watahakikisha uwanja wa Sokoine unakarabatiwa ikiwa ni pamoja na kujenga.mashindano ya Umoja Cup yaliyodhaminiwa na Serengeti Media Centre,Kampuni ya Sijui Kitu na Mageta yanatarajiwa kukamilika agosti 8 mwaka huu ambapo mshindi wa kwanza anapata Ng'ombe na Mpira ,wa pili Mbuzi na Mpira wa tatu Mipira miwili na wanne mpira mmoja ,zawadi hizo zimeongezeka baada ya Mbunge wa Jimbo hilo kwa kuguswa ametoa mipira minne na kuahidi kuwa anatarajia kuanzia ligi yake itakayoshirikisha wilaya nzima.Aidha Pama Bazaar ameahidi kutoa sh 50,000 kwa mfungaji bora na Chuo cha Utalii cha Serengeti(SETCO)wameahidi kutoa sh 40,000 kwa timu bora na wanategemea kununua kikombe kwa ajili ya timu bora ,wadau walio tayari kutoa zawadi wanakaribishwa






0 comments:

Post a Comment