Fahari ya Serengeti

Tuesday, August 2, 2016

WAUMINI WA KANISA LA KANISA LA MENONITELA KIINJILI (KMKT MUGUMU WAHITIMISHA MKUTANO WA VIBANDA


Wanakwaya kutoka Musoma kaskazin wakitumbuiza waumini katika mkutano wa vibanda(KMKT)Mugumu mjini
Askofu Mkuu wa Dayosisi Mara(KMKT) Naamon Kajeri akiwahubiri waumini katika moja ya ibaada za mkutano wa makambi jimboni Mugumu.
Mama Askofu Ester Kajeri akiwasalimu washiriki katika ibaada maalum ya mkutano.
Askofu Mkuu Dayosisi ya Mwanza Lameck Manji(kushoto)na Mchungaji Paulo Budaga wakisikiliza mafundisho ya ibaada katika mkutano wa vibanda jimboni Mugumu.


Mchungaji Mtatiro akiwafundisha washiriki wa KMKT kuhusiana na umuhimu wa Maombi.
Baadhi wa viongozi wa kanisa la KMKT wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuhitimisha mkutano wa vibanda katika jimbo la Mugumu mjini.
Wakati wa harambee watu wengi walijitokeza kuhakikisha kazi ya Mungu inaenda vizuri.
Kikundi cha kwaya kutoka Musoma Kusini nao walikuwepo kuhakikisha kazi ya Mungu inatendeka sawasawa.
Askofu Mkuu Naamon Kajeri akiwasalimia wageni na wenyeji katika ufumbuzi wa mkutano wa vibanda uliofanyika katika kanisa la Menonite la kiinjili Tanzania(KMKT)Mugumu mjini.
Wapigaji wa vyombo vya Muziki wakisikiliza mahubiri yaliyokuwa yakiendelea katika mkutano.
Washiriki na wakristo wa madhehebu mbalimbali wakifuatilia mahubiri katika mkutano uliofanyika jimboni Mugumu(KMKT).
Kiongozi wa nyimbo za Tenzi akiwaongoza waumini kumwabudu Mungu kwa njia ya nyimbo.
Waumini wakitoa sadaka zao kama shukurani ya ibaada katika mkutano wa vibanda(KMKT)
Askofu kiongozi Dayosisi ya Mara Naamon Kajeri(kulia)akimkaribisha Askofu Lameck Manji mbele ya madhabahu kwa ajili ya kuhubiri Neno la Mungu katika mkutano.
Askofu mkuu wa kanisa la (KMKT) Dayosisi ya Mwanza Lameck Manji akihubiri neno la Mungu mbele ya washiriki.
Baadhi ya waumini wakiendelea kupata mahubiri kutoka kwa Askofu Lameck Manji.
wapigaji wa vyombo wakiendelea kutoa huduma ya kusifu kwa njia ya nyimbo.
Washiriki wakipeana mkono wa baraka mara baada ya kuhitimisha ibaada ya mkutano wa vibanda.


0 comments:

Post a Comment