Fahari ya Serengeti

Tuesday, August 2, 2016

MBUNGE SERENGETI AUNGANA NA WADAU WENGINE KUTOA ZAWADI KWA TIMU NNE BORA LIGI YA UMOJA CUP

 Mbunge wa Jimbo la Serengeti Marwa Ryoba ameahidi kutoa zawadi ya mipira minne kwa ajili ya washindi wa kwanza hadi wa nne Ligi ya Umoja Cup,ahadi hiyo ameitoa wakati anaongea na Serengeti Media Centre ambao ni Miongoni mwa waandaaji wa ligi hiyo iliyokuwa inashirikisha timu 12 ,na kati ya hizo timu sita zimeingia robo fainali ambayo inatarajiwa kuanza agosti 3 kwa kuzikutanisha timu za Smart boy's fc na Itununu Fc,itakayoanza saa nane uwanja wa Sokoine na mchezo wa pili ni kati ya Mageta Fc na Burunga Fc.
Mbunge amesema ameamua kutoa zawadi hizo kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za waandaaji ambao ni pamoja na kampuni ya Sijui Kitu na Mageta ,na kuwa yeye anatarajia kuandaa ligi itakayoshirikisha timu zote za wilaya.
Kutokana na ahadi ya Mbunge ambayo amesema wakati wowote atatoa mshindi wa kwanza sasa atapata ng'ombe na mpira mmoja,wa pili mbuzi na mpira,watatu mipira miwili na wa nne mpira mmoja.
wakati huo Chuo cha Utalii Serengeti Setco wameahidi kutoa sh 40,000 kwa timu bora na wanaendelea kutafuta kikombe kwa ajili ya timu bora,na pia wanajitahidi kuhakikisha wanatoa zawadi kwa kipa bora,naye Paulo Magoiga(Pama Bazaar )ameahidi kutoa sh 50,000 kwa ajili ya mfungaji bora.
Waandaaji wanaomba wadau mbalimbali wajitokeze kutoa zawadi kwa kuwa bado zawadi ya waamzi,na timu itakayokuwa imeonyesha nidhamu bora.


0 comments:

Post a Comment