viwanja vya shule ya msingi Mugumu B,
Wanafuatilia michezo na nasaha mbalimbali kutoka kwa viongozi wa wilaya ya Serengeti.
Mabango yenye jumbe mbalimbali yalikuwepo.
Maigizo yenye ujumbe kwa jamii na watoto yametolewa,wamesisitiza kuepuka ukatili wa kijinsia kwa watoto,ndoa za utotoni,ukeketaji na mimba kwa wanafunzi ili wapewe elimu.
Viongozi mbalimbali wakijadiliana mambo wakati burudani zikiendelea.
Katibu Tawala wilaya ya Serengeti Cosmas Qamara akikagua banda la vifaa mbalimbali vinavyotengenezwa na watoto waliokimbia kukeketwa na kuhifadhiwa katika kituo cha Nyumba Salama Mugumu Serengeti.
Dc Serengeti Nurdin Babu akitoa hotuba ambapo amezitaka mahakama na Polisi kuharakisha kesi zinazohusiana na ukatili wa kijinsia ikiwemo mimba kwa watoto,ukeketaji,ndoa za utotoni,vipigo ,ulawiti,ubakaji ,kwa kuwa jamii inakata tamaa kwa jinsi zinavyoendeshwa kwa muda mrefu.
Bonanza la michezo limefanyika kwa mpira wa miguu wasichana na wavulana.
Zawadi zimetolewa kwa waliofanya vizuri.
Wataalam wa mitambo wako kazini kuhakikisha mambo yanasikika vema.
Mtoto huyo alipata dhoruba wakati wa maadhimisho hayo na kupoteza fahamu,hata hivyo alipata ahueni.
0 comments:
Post a Comment