Fahari ya Serengeti

Friday, June 9, 2017

UCHIMBAJI DHAHABU MERENGA SERENGETI WENYE LESENI WAKATALIWA NA WANANCHI

 Wakazi wa kijiji cha Merenga wilaya ya Serengeti wakiwa kwenye mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na Mbunge wa Jimbo hilo Marwa Ryoba na Mwanasheria wa Halmashauri wamesema hawatawaruhusu watu waliopewa leseni ya kuchimba dhahabu kijijini hapo kwa kuwa wenye mashamba wameishashirikishwa,wamekubaliana kuwa serikali ya kijiji ikate leseni na wananchi wachimbe kupitia kwenye vikundi vyao.
Mbunge wa jimbo la Serengeti Marwa Ryoba wa pili kulia akiwa kwenye mkutano wa hadhara wa wananchi wa Merenga ambapo alikwenda kwa ajili ya kusikiliza matatizo yao kufuatia mvutano kati ya wenye mashamba,wananchi na waliopewa leseni ya uchimbaji dhahabu kijijini hapo.

Hata hivyo imebainika kuwa wenye leseni hawakuwashirikisha wenye maeneo,na hawana muafaka ,hivyo wameazimia kuwa leseni yao ifutwe ili serikali ya kijiji ikate leseni na wananchi kupitia vikundi vyao wachimbe,wa kwanza kulia ni Mwanasheria wa Halmashauri Veronica Luvanda,wa kwanza kushoto ni afisa mtendaji wa kijiji, na Kaimu Mwenyekiti wa kijiji,Picha zote Serengeti Media Centre.

0 comments:

Post a Comment