Fahari ya Serengeti

Thursday, July 30, 2015

GIZ YATOA VIFAA KWA HALMASHAURI YA SERENGETI

Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara Naomi Nnko akiwa na wataalam wa halmashauri hiyo wakipokea msaada toka shirika la Kijermani (GIZ)linaloshughulika na masuala ya maliasili katika halmashauri hiyo
Mkurugenzi wa shirika la GIZ Afrika Mashariki Martin Miiller akikabidhi kifaa cha kupimia ardhi,Total Station Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo  chenye thamani ya sh 27.3 mil.kwa ajili ya kupima viwanja,na mipaka.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti Naomi Nnko akiwa ameshikilia Total Station,kulia Mkurugenzi wa shirika hilo Tanzania Regine Qualmann akijiandaa kumkabidhi mashine mbili za GPS.
Regine Qualmann akimkabidhi Ded Nnko Gps mbili kwa ajili ya idara ya ardhi zenye thamani ya sh 3,980,000
Shirika hilo limekabidhi Printer ya kisasa kwa ajili ya idara ya Maliasili
Ded na afisa ardhi na Maliasili wilaya Jonas Nestory wakiwa na Printer baada ya kukabidhiwa.




KUDHIBITI MIGOGORO YA WANYAMA NA WANANCHI IDARA YA WANYAMAPORI KUPEWA GARI,
Serengeti:Shirika la Kijermani linaloshughulika na masuala ya Maliasili Tanzania(GIZ) linatarajia kutoa gari ,trekta na vifaa vya doria kwa halmashauri ya wilaya ya Serengeti ili kudhibiti wanyama wanaovamia mashamba ya wananchi.
Afisa wa shirika Afrika Mashariki Martin Miiller akikabidhi vifaa vya kupimia ardhi,viwanja , Gps 2 na Printa ya kisasa vyenye thamani ya zaidi ya sh 32 milioni kwa halmashauri ya wilaya ya Serengeti jana,alisema lengo ni kuijengea uwezo wa kusimamia masuala ya ardhi,Maliasili kwa jamii.
Alisema ili kupunguza migogoro kati ya jamii na wanyama shirika lao linatarajia kuikabidhi halmashauri hiyo gari jipya na vifaa kwa ajili ya doria ,lengo likiwa ni kuendelea kulinda na kuhifadhi Maliasili hizo ambazo zinafaida kwa jamii na Taifa.
“Katika Ikolojia ya Serengeti tunafanya kazi katika wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara  na Ngorongoro Mkoa wa Arusha…lengo likiwa ni kuhakikisha ikolojia hiyo inalindwa na kuendelea kustawi,lakini kwa maeneo mengine tunafanya kazi katika sekta za afya,huduma ya maji kwa mikoa ya Tanga,Mbeya na Dar es salaam,”alisema.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa shirika hilo hapa Tanzania Regine Qualmann alisema wameishatoa magari manne manne  kwa hifadhi ya Taifa ya Serengeti ,shirika la Frankurt Zoological Society(FZS)na halmashauri ya Ngorongoro ,lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kulinda na kuhifadhi Maliasili hizo.
Akipokea msaada huo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Naomi Nnko alisema ,kupitia mpango huo itawasaidia kuboresha huduma kwa jamii ikiwa ni pamoja na kuboresha makazi yao kwa kujenga nyumba za kisasa.
Afisa wanyamapori halmashauri hiyo John Landoyan alisema msaada wa gari utawasaidia kutatua matatizo ya wananchi kwa wakati na kupunguza migogoro kati ya wahifadhi na jamii,kwa kuwa wamekuwa hawawezi kufanya doria kutokana na tatizo la gari na vifaa vya doria.
Akizungumzia umuhimu wa vifaa walivyokabidhiwa afisa ardhi na Maliasili wilaya Jonas Masingija alisema kifaa cha kupimia ardhi kitasaidia kupima vijiji na viwanja ili kupunguza migogoro ya mipaka kati ya wananchi na maeneo yaliyohifadhiwa.
Katika halmashauri hiyo shirika hilo limejikita katika kujenga uwezo kwa halmashauri na jamii kwa masuala ya Maliasili ,na utawala bora.
Mwisho.



Wakuu wa idara wakishuhudia makabidhiano hayo

Ded akiwa na GPS
Uongozi wa halmashauri ukiwapa zawadi viongozi wa GIZ baada ya kukabidhi vifaa vyenye thamani ya zaidi ya sh 31.8 milioni.
Hii ni zawadi tunayokutunuku watu wa serengeti





1 comment:

  1. Asanteni kwa kutuhabarisha ila mpo kimyaa saaana msiandike ya mjini tuu chimbueni serengeti ni kubwa ingieni hadi vijijini huko kuna makubwa zaidi yanapaswa kuhabariswa
    0784660623 nyakitono home

    ReplyDelete