Fahari ya Serengeti

Wednesday, August 2, 2017

VIJIJI VINAVYOUNDA JUMUIYA YA IKONA VYAPOKEA MAMILIONI YA FEDHA

 Viongozi wa Ikona Wma wilaya ya Serengeti wakiwa na viongozi wa vijiji wanachama wa jumuiya hiyo inayounda na vijiji vya Robanda,Parknyigoti,Nyichoka,Nattambiso na Makundusi wamepokea hundi ya zaidi ya sh 172 mil kwa kila kijiji ,ikiwa ni mgao wao wa fedha zilizotokana na mapato wanayokusanya,fedha hizo hutolewa asilimia 50 ya mapato yote kurudi kwa jamii ili kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo.
 Katibu wa Ikona Wma Yusuph Manyanda akitoa ufafanuzi wa mgao wa fedha kwa wajumbe,katikati ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Elias Nchama na pembeni ni Makamu Mwenyekiti Jakobo Bega
 Wahenga wanasema penye jambo zuri kila mmoja hufurahi wanapiga makofi kuonyesha wanakubaliana na taarifa iliyotolewa.
 Viongozi wanafuatilia taarifa kwa makini
 Wengine wanakokotoa mahesabu na kuweka kumbukumbu sawa kwa kila hatua
 Mambo mazuri wanaonekana wakisema

 Picha ya Pamoja haikusahaulika

 Anachangia hoja
 Msisitizo ulitolewa na viongozi
Zote zimeenda vijijini

0 comments:

Post a Comment