Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti Juma Porini katikati akijadiliana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Juma Hamsini kushoto na Mbunge wa jimbo hilo Marwa Ryoba baada ya kubainika kuwa kanuni za kikao cha madiwani zimekiukwa na wataalam kwa kushindwa kuwasilisha taarifa ya mwaka ambayo ingejadiliwa katika kikao hicho cha kawaida.
Katika kikao hicho madiwani walipaswa kuchagua makamu mwenyekiti,wenyeviti wa kamati,kuunda kamati na kupitisha ratiba ya vikao vya mwaka,kutokana na mapungufu hayo kikao kimeahirishwa huku wakiazimia kuchukua hatua kwa wataalam waliohusika kwa kuwa wanasababishia halmashauri hasara.
Dc Nurdin Babu akijadiliana na Mwenyekiti wa halmashauri Juma Hamsini,Mbunge wa jimbo hilo Marwa Ryoba na Mkurugenzi Mtendaji Juma Hamsini ili kunusuru jahazi,hata hivyo kikao hicho kimeahirishwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Serengeti Juma Hamsini akitoa maelezo ya kikao kabla ya kufunguliwa.
Madiwani na wataalam wakifuatilia mjadala kikao kifanyike ama la,hata hivyo kimeahirishwa
Diwani wa Mugumu Joseph Kihungwe(Mchina )ameacha dude na kusababisha kikao kuahirishwa baada ya kubainika kanuni zimekiukwa
Madiwani n je ya kikao wakijadiliana
Mijadala kila kona iimefanyika baada ya kupata muda wa mapumziko ili mambo yawekwe sawa,hata hivyo uamzi wa mwisho kikao kimeahirishwa
Thursday, August 3, 2017
Home »
» KUKOSEKANA KWA TAARIFA YA MWAKA KWASABABISHA BARAZA KUAHIRISHWA
0 comments:
Post a Comment