Fahari ya Serengeti

Thursday, August 10, 2017

JUMA PORINI CUP YAWALETA PAMOJA WAKAZI WA NATTA SERENGETI


Diwani wa Kata ya Natta wilaya ya Serengeti ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo Juma Porini mwenye shati la draft akiwa na viongozi na wachezaji wa timu mbalimbali za mpira wakati wa Kombe la Porini Cup ,
Mashindano hayo ambayo yameshirikisha timu 12 za mpira wa miguu ,mbio za magunia,kufukuza kuku,mbio za baiskeli ,mbio ndefu na netibali na kufuatiwa na utoaji wa zawadi za zaidi ya sh 8 mil kwa washindi wote ikiwemo wachezaji ,waamzi na kamati ya maandalizi.
Aidha katika mashindano hayo wamefanikiwa kuunda timu ya mpira wa miguu kata ya Natta ambayo amesema atakuwa mlezi wake.

Nahodha wa timu ya netiboli ya Natta Sekondari wilaya ya Serengeti Jakline akipokea kombe kutoka kwa mgeni rasmi kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri Wambura Sunday baada ya kuibamiza timu ya Grumeti kwa mabao 13-4 na kuibuka bingwa Juma Porini Cup.
 Wachezaji wa timu ya Grumeti Fc wakiwa katika picha ya pamoja.
 Mgeni Rasmi Wambura Sunday akikagua timu ya netiboli ya Grumeti kabla ya kupokea kichapo kutoka kwa vijana wa  Natta sekondari kwa  magoli 13-4
 Burudani mbalimbali zilihanikiza katika kwenye mashindano ya Porini Cup
 Mmabo yanaenda yakiongezeka,watu wa rika mbalimbali wameshiriki
 Mwali aking'ara akisubiri mlengwa
 Porini Cup imewaleta pamoja watu mbalimbali,hapo ni jaza ujazwe wanapigwa picha na kupiga picha,
 Zawadi zikitolewa

 Kila mtu anavuna alichopanda zawadi zinazidi kumiminika


 Washabiki walikuwa lukuki




Zawadi zawadi ni jaza ujazwe bandika bandua

0 comments:

Post a Comment