Baadhi ya wazee wa koo ya Inchugu kata ya Machochwe wilaya ya Serengeti wakiweka sahihi ya makubaliano ya kuachana na ukeketaji katika koo hiyo ,uamzi huo umefikiwa na kutangazwa kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Nyamakendo.
Wasanii wa Nuru Sanaa wakitoa elimu ya madhara ya ukeketaji kwa watoto wa kike katika kijiji cha Nyamakendo muda mfupi kabla wazee wa mila hawajatoa tamko. |
Wasanii wakiendelea kutoa elimu ya madhara ya ukeketaji
Meneja Mradi wa Tokomezza Ukeketaji Serengeti Godfrey Matumu akiweka saini baada ya wazee wa mila kukamilisha zoezi la kusaini makubaliano ya kukataa ukeketaji na kuanza mikakati ya jando bila ukeketaji.
William Mtwazi(Mwanasheria)kutoka LHRC ambaye ni afisa mradi wa Tokomeza Ukeketaji Serengeti akitoa ufafanuzi kwa wazee wa mila wa koo ya Inchugu namna ya kusimamia maamzi yao ya kupiga marufuku ukeketaji na kuanza jando bila ukeketaji
Wazee wa mila na viongozi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja
Mjadala unaendelea wao kwa wao na hatimaye wakatoka na tamko la kupiga marufuku ukeketaji
Anasaini makubaliano yao ya kupiga marufuku
Wanaendelea kusaini
Watoto wameshuhudia makubaliano ya wazee wa mila kisha kutoa tamko ambalo linawaweka huru watoto wa kike ambao wengi wakati wa msimu wa ukeketaji hukimbia na kutafuta hifadhi maeneo mengine.
Biashara inaendelea lakini wakisikiliza msimamo wa wazee wa mila
Wanafuatilia mkutano wa wazee wa mila huku biashara ikiendelea
Hawa wote wameshuhudia tamko la wazee wa mila,huku wanawake wakidai kuwa kama hawatabadilika familia nyingi zitaishi kwa amani kwa kuwa kumekuwa na migogoro mingi wakati wa ukeketaji ukifika ambapo wanawake wanaowatetea watoto wao wamekuwa wakifukuzwa nyumbani
Kisha biashara zikaendelea kama kawaida
0 comments:
Post a Comment