Askofu Michael Msonganzila wa Jimbo Katoliki la Musoma akiongea na Josephina Bakhita wa Jumuiya ya Mtakatifu Maria Mama wa Mungu Parokia ya Mugumu wilaya ya Serengeti baada ya kusali misa katikaJumuiya hiyo na kumwombea na kumpa baraka mama huyo ambaye anasumbuliwa na magonjwa ya sukari na Moyo,katika ibada hiyo iliyohudhuriwa na waumini wa jumuiya mbalimbali wakiongozwa na Kwaya ya Mt,Fransisco wa Asizi Parokia ya Mugumu,amehimiza wanajumiya kuyaishi maisha ya somo wao Bikra Maria ya upole,unyenyekevu na imani huku wakiwaombea na wengine.
Baba askofu Msonganzila yuko katika ziara ya siku nne ya kichungaji katika Parokia hiyo ambapo mbali na shughuli nyingine atatoa Kipaimara kwa watu zaidi ya 400.
Baba Askofu Michael Msonganzila akitoa maombi na baraka kwa Josephina Bakhita.
Baba Askofu Michael Msonganzila akiongoza sala ya baraka kumwombea Josephina Bahkita,kushoto ni Paroko wa Kanisa katoliki Mugumu Alois Magabe na Sista Rozina Massawe.
Saturday, August 26, 2017
Home »
» ASKOFU MSONGANZILA AHIMIZA WANAJUMUIYA KUISHI MAISHA YA KIKRISTO
0 comments:
Post a Comment