Fahari ya Serengeti

Wednesday, August 23, 2017

WAZIRI APOKEA MRADI WA NYUMBA ZA SH 1.4 BILIONI

Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe  kushoto,Balozi wa Ujermani nchini Tanzania  Dk Detlef Wachter katikati na Afisa Ujilani Mwema shirika la Frankfurt Zoological Society Masengeri Tumbuyo kulia wakikata utepe kama ishara ya kuzindua nyumba nne za watumishi na ofisi tatu za watumishi wa Idara ya Ujilani Mwema Hifadhi ya Taifa ya Serengeti zilizojengwa kwa Ufadhili wa Serikali ya Ujermani  kupitia Benki ya Maendeleo ya nchi hiyo KFW kwa thamani ya sh 1.4 bil,lengo likuwa ni kuhakikisha watumishi wengi wanahamia Fort Ikoma ambako ni nje ya  ili kulinda na kuhifadhi Mfumo wa Ikolojia ndani ya Hifadhi hiyo.



 Meneja Mahusiano wa Tanapa (mc)wa shughuli hiyo Paskael Shelutete akisoma maandishi yaliyoandikwa kwenye jiwe la Msingi mara baada ya Waziri na Balozi kukabidhiana nyumba hizo.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe akipokea funguo za nyumba nne na ofisi tatu toka kwa Balozi wa Ujermani hapa nchini Dk Detlef Watchter zilizjengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Ujermani kwa thamani ya sh 1.4 bilioni kwa ajili ya wafanyakazi wa Idara ya Ujilani Mwema hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

 Waziri akiangalia mashine aina ya Hydroform ambayo wanaitumia kufyatua matofali ya gharama nafuu na ambayo hayachomwi kwa ajili ya kuhifadhi mazingira,mashine hiyo ina uwezo wa kufyatua matofali 3000 kwa siku,inatumia mafuta ya dezeli lita 10 kwa siku.


 Wnashiriki zoezi la kufyatua matofali
 Wakiangalia matofali yaliyokwisha fyatuliwa
 Waziri Maghembe akimakbidhi funguo za nyumba nne na ofisi tatu Mkurugenzi wa Tanapa Allan Kijazi baada ya kukabidhiwa na Balozi wa Ujermani hapa Nchini.
 Burudani kutoka kikundi cha COCOBA Bonchugu ilikonga nyoyo za watu
 Waziri akikagua nyumba na ofisi kabla ya kuzindua

 Balozi wa Ujermani hapa nchini Dk Detlef Wachter akiwa na tofali alilofyatua kwa mashine ya Hydraform

 Moja ya nyumba ya watumishi iliyokabidhiwa

 Wasomee jiwe limeandikwaje?
 Mc Shelutete akifanya yake
 Wanafuatilia taarifa kutoka kwa viongozi mbalimbali

 Asante sana kwa msaada wa nyumba tunaomba mkamilishe mpango wa maji kutoka Borogonja na kituo cha Taarifa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti anasikika akisema Waziri
 Picha mbalimbali za pamoja zilipigwa

Walizungukia maeneo

0 comments:

Post a Comment