Timu ya Mugumu Star (Wahenga) imeanza ligi ya Mapesa Cup kwa kuwabana vijana machachari wa Rwamchanga Fc na kulazimisha sare ya kutofungana na kugawana pointi moja moja kwenye Uwanja wa Sokoine Wilaya ya Serengeti.
Ligi hiyo ya Mapesa Cup itashirikisha timu 14 kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo inatarajiwa kukamilika septemba 13 mwaka huu,ambapo mshindi wa kwanza ataibuka na ng'ombe wawili,mshindi wa pili ng'ombe mmoja na mshindi wa tatu mbuzi wawili.
Pia kutakuwa na zawadi mbalimbali kwa ajili ya kipa bora,mfungaji bora na waamzi.
Kwa mjibu wa Emmanuel Mapesa mdhamini wa ligi hiyo alisema kwa kushirikiana na walimu wenzake wameanzisha ligi hiyo kwa lengo la kuibua vipaji na kuwapa uzoefu waamzi waliomaliza mafunzo hivi karibuni.
Mugumu Star (wakongwe) wenye sare za bluu wakionyeshana ubabe na vijana wa Rwamchanga Fc uwanja wa Sokoine katika kuwania kombe la Mapesa.
Wednesday, August 9, 2017
Home »
» MAPESA CUP WAHENGA MUGUMU STAR YAWABANA RWAMCHANGA FC
0 comments:
Post a Comment