Fahari ya Serengeti

Friday, August 4, 2017

UKOSEFU WA OFISI YA WALIMU SERENGETI SEKONDARI WAFANYIA KAZI CHINI YA MTI

Walimu wa shule ya sekondari Serengeti wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa ofisi hali ambayo inawalazimu kufanyia kazi zao chini ya mti na wakati wa mvua hulazimika kukimbilia kwenye vyumba vya madarasa.
Oktoba mwaka jana bweni la wasichana katika shule hiyo liliungua na kusababisha watoto kukosa sehemu ya kulala na kuwalazimu walimu kupisha ofisi yao itumike kama bweni kwa ajili ya wanafunzi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Juma Hamsini amesema kuwa wanamkakati wa ujenzi wa bwalo la chakula na ofisi ya walimu ili waweze kutoka katika mazingira hayo.
Shughuli zinaendelea kama kawaida

0 comments:

Post a Comment