Fahari ya Serengeti

Friday, March 31, 2017

KESI YA NGARIBA YAPIGWA TAREHE

SERENGETI MEDIA CENTRE
Ngariba Wansato Buruna kushoto akiwa mahakamani ,kulia ni mwenzake ambao wanashitakiwa kwa makosa ya kukeketa watoto.

Kushindwa kufika mahakamani kwa watoto ambao ni wanafunzi kumesababisha kesi  tano  za jinai zinazomkabili  Ngariba Wansato Buruna(56)na wenzake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara kuahirishwa.

Watoto ambao wanaendelea na mitihani kwa ajili ya likizo fupi walitakiwa na mahakama hiyo kuwasilisha ushahidi wao dhidi ya ukatili unaodaiwa kufanywa na ngariba huyo na wenzake  mwishoni mwa mwaka jana ambao walikeketwa na kisha kukamatwa na askari polisi na kuwataja washitakiwa kuwa ndiyo waliohusika.

Hata hivyo hakimu wa Mahakama hiyo Ismael Ngaile ameahirisha kesi hiyo hadi aprili 21 mwaka huu.

Aidha uamzi mdogo uliotakiwa kutolewa Katika shauri namba 234/2016 dhidi ya Wansato Buruna(56) na Bhoke Mseti(40) wanaotetewa na wakili Baraka Makowe haukutolewa hadi 

aprili 21 mwaka huu,na Mahakama imempa dhamana mshitakiwa  Bhoke Mseti baada ya kutimiza vigezo na masharti ya dhamana ya sh 5 milioni ya maneno na wadhamini wawili.

Mwisho.

0 comments:

Post a Comment