Fahari ya Serengeti

Thursday, March 30, 2017

MWENYEKITI WA SERIKALI YA KIJIJI CHA BORENGA AKATALIWA NA WANANCHI

Wajumbe wa serikali ya kijiji cha Borenga kata ya Kisaka wilayani Serengeti wakiwa wamekaa chini ya mti hawana la kufanya kufuatia afisa mtendaji wa kata hiyo Mturi Sausi kuingia mtini baada ya kubaini kuna waandishi wa habari wanafuatilia sakata la Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Julius Maro kukataliwa na wananchi na yeye kutangaza kung'atuka lakini ameendelea kukalia ofisi huku akidaiwa kufanya hujuma mbalimbali ikiwemo uuzaji wa ardhi kwa wakazi wa Tarime.

Mtendaji huyo alikuwa ameitisha kikao cha Serikali ya kijiji kwa ajili ya kujadili mgogoro wao na mwenyekiti uliopelekea kumkataa mara mbili na kufuatiwa na mkutano mkuu wa kijiji kumkataa,hata hivyo baada ya kupata taarifa za uwepo wa waandishi wa habari kijijini hapo hakuweza kutokea na kusababisha wajumbe kukaa chini ya mti kwa muda mrefu wakimsubiri bila mafanikio.

Mkuu wa wilaya hiyo Nurdin Babu ameahidi kwenda kijijini hapo kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero hiyo ambayo imechangia shughuli za maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule kukwama kwa kuwa wananchi wamegoma kuchanga mpaka mwenyekiti awasilishe fedha zinazolipwa na mchimbaji mdogo wa dhahabu zaidi ya sh 6 mil,.

Jengo la shule ya Msingi Borenga ambayo imekwama kujengwa kutokana na mgogoro uliopo kati ya wananchi na mwenyekiti wa kijiji ,hata hivyo wananchi wanamtaka Mkurugenzi Mtendaji kupeleka mtendaji wa kijiji kwa kuwa maafisa kilimo wanaokaimu mara kwa mara wanadaiwa kuwa sehemu ya hujuma ya rasilimali za kijiji.
Baadhi ya wachimbaji wadogo wakiwa katika eneo lao la kazi ,mgodi huo unaodaiwa kuwa chini ya kijiji mchimbaji aliyeingia makubaliano na serikali ya kijiji anadaiwa hajalipa zaidi ya sh 6 mil,Mwenyekiti wa kijiji akidaiwa kumkingia kifua.

0 comments:

Post a Comment