Fahari ya Serengeti

Thursday, March 9, 2017

MAADHIMISHO YA SIKU YA MWANAMKE,NGARIBA WATAKIWA KUACHA KUWAFANYIA UKATILI WATOTO WAO.

 Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu amewataka wanawake kuwa chachu ya mabadiliko kwa kuachana na vitendo vya ukeketaji wa watoto wa kike ,kwa kuwa wamekuwa vinara wa kuwafanyia ukatili watoto wao.
Amesema hayo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mwanamke Duniani yaliyofanyika  kiwilaya katika kijiji cha Nyamakendo kata ya Machochwe,ambapo amesema wanawake ndiyo ngariba na ndiyo wanafanya maandalizi yote,hivyo wanatakiwa kubadilika kifikra kwa kuwasomesha watoto wao ili kufikia lengo la serikali ya awamu ya tano ya kujenga Tanzania ya viwanda.

Amewataka wazee wa mila kuacha kukumbatia mila zenye madhara kwa watoto wa kike na badala yake wawekeze kwenye elimu ambayo itasaidia kuharakisha maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
 wanafunzi wa shule ya sekondari Machochwe wakitoa Burudani kwa wageni walioudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya mwanamke.
 Wageni kutoka nchi mbalimbali za kigeni wakifatilia tukio zima la siku ya mwanamke Duniani katika viwanja vya Nyamakendo kijijini Machochwe.

 Wazee wa mila nao walikuwa wakiwa makini kuhakikisha ujumbe unawafikia katika siku maalum ya wanawake iliyoadhimishwa kijijini Machochwe.
 Wanafunzi kutoka shule mbalimbali wakifatilia matukio yaliyofanyika katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake kijijini Machochwe.
 Kikundi cha Ritungu kikiwa kimemaliza kutoa burudani kwa wananchi waliohudhuria kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika kijiji cha Machochwe.
 Kikundi cha kwaya ya wanafunzi kikitoa  burudani ya nyimbo kwa wananchi waliohudhuria sherehe hizo
 Mabinti wa kisasa kutoka Nyumba Salama wakitumbuiza katika siku ya wanawake kiwilaya iloyofanyika kijijini Machochwe.

 Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu akisalimiana na wananchi baada ya kuwasili katika viwanja vya Nyamakendo kwa ajili ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani.

 Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu akiwapongeza wanamichezo wa shule mbalimbali baada ya kucheza katika viwanja vya shule ya msingi Nyamakendo.
 Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu akipeana mikono na wachezaji waliofika kuadhimisha siku ya mwanamke duniani.
 Wananchi wakiendelea kufatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea katika viwanja vya shule ya msingi Nyamkendo kwenye siku maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
 Mwanafunzi akipokea zawadi ya mpira baada ya kuibuka mshindi katika mechi zilizochezwa kwenye siku ya wanawake duniani kijijini Machochwe.
 Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu akiteta jambo na binti mchezaji katika uwanja wa Nyamakendo baada ya Mechi kuchezwa.
 Mwanamichezo wa mpira wa mikono akipokea zawadi ya mpira baada ya ushindi walioupata  katika moja ya mechi kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.

0 comments:

Post a Comment