Uzinduzi wa
mazoezi ili kuzuia magonjwa yasiyo ya kuambukiza wilaya ya Serengeti Mkoa wa
Mara kufanyika machi 11 mwaka huu .Mpango
huo ambao ni agizo la Makamu wa Rais
Samia Suluhu ambapo kila jumamosi ya pili ya mwezi ni siku ya mazoezi
ya viungo ili kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukizwa,unaratibiwa na
ofisi ya mkuu wa wilaya.
Taarifa ya
Katibu Tawala Wilaya Cosmas Qamara kwa vyombo vya habari inabainisha kuwa
mazoezi yataanzia ofisi ya Mkuu wa wilaya na kuishi Uwanja wa michezo wa
Sokoine ambapo mazoezi mbalimbali ya viungo yatafanyika.
Kwa mjibu wa
taarifa hiyo inabainisha kila taasisi inatakiwa kushiriki kikamilifu mazoezi
hayo na kuratibu ushiriki wa watumishi wake baada ya mazoezi kukamilika.
Kwa upande
wa vijijini amewaagiza viongozi ikiwa ni
pamoja na watendaji waratibu elimu kata
kutoa taarifa katika ofisi yake machi 12 mwaka huu kuhusiana na ushiriki wa
jamii .
Hata hivyo
baadhi ya wakazi wa mji wa Mugumu wamesema uzinduzi wa mazoezi hayo utasaidia
viongozi kuchukua hatua dhidi ya watu waliovamia maeneo ya wazi ambayo yalikuwa
wakisaidia vijana kufanya mazoezi mbalimbali ya viungo.
0 comments:
Post a Comment