Serengeti Media Centre.
Joseph Nyiboha(22)mkazi wa kijiji cha Borenga wilayani
Serengeti Mkoani Mara amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kubaka na kumpa mimba mwanafunzi
aliyekuwa amechaguliwa na kujiunga na kidato cha kwanza Machochwe sekondari.
Hata hivyo mshitakiwa
wakuwepo mahakamani kwa kile kinachodaiwa kuwa alitoroka baada ya kudhaminiwa.
Kabla ya kutolewa adhabu hiyo mwendesha mashitaka wa Jamhuri
Jakobo Sanga Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa wilaya Ismael Ngaile akisoma maelezo katika kesi ya jinai namba
87/2016 ,alisema mshitakiwa alifikishwa mahakamani akikabiliwa na makosa matatu
ya jinai.
Alitaja kosa la
kwanza kuwa ni kuishi na mwanafunzi kinyume na kifungu 134 cha Sheria ya Elimu
sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, na kosa la pili ni
kumbaka mwanafunzi wa miaka 15 aliyetarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza
Machochwe sekondari 2016 ikiwa ni kinyume na kifungu namba 130(1)na(2)(e)na
namba 131(1)cha sheria ya ubakaji sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho
mwaka 2002.
Sanga aliiambia Mahakama kuwa kosa la tatu ni kumpa mimba mwanafunzi kinyume na kifungu
namba 35(3)na(4)sheria ya Elimu sura ya 353 kama ilivyofanyiwa marekebisho
mwaka 2002.
Mshitakiwa alikamatwa Oktoba 24 mwaka 2015 nyumbani kwake katika
kijiji cha Borenga baada ya kubainika
kuishi na Mwanafunzi wa shule ya msingi Borenga aliyekuwa amechaguliwa kujiunga
na kidato cha kwanza Machochwe,hata
hivyo alikuwa tayari ni mjamzito,na kuomba adhabu kali itolewe.
Hakimu Ngaile alisema
ushahidi uliotolewa mahakamani haukuacha
shaka”mahakama yangu inatoa adhabu kali kwa mshitakiwa ,katika kosa la kwanza atatumikia
kifungo cha miaka 5 jela, kosa la
pili kifungo cha miaka 30 jela na kosa la tatu atakwenda jela miaka 30
adhabu zote zitakwenda pamoja atatumikia miaka 30”alisema.
mwisho.
0 comments:
Post a Comment