Mnanka Godfrey Chacha Mtoto aliyegeuka mlezi wa Familia (katikati)akiwa darasani Sekondari ya Kambarage baada ya kusaidiwa na wasomaji wa gazeti la Mwananchi kwa kupata fedha ambazo zimemwezesha kununua mahitaji ya shule,nyumbani kwa ajili ya yeye na wadogo zake.pamoja na kuwa analazimika kutembea kilometa 14 kwa mguu kila siku kwenda shule na kurudi ameahidi kusoma kwa bidii,huku akiwashukuru walioguswa na matatizo yake na kuwaomba watu kuendelea kuwasaidia ili wadogo zake waweze kuanza shule.
Pia mahali pa kuishi kwa kuwa nyumba wanayoishi kwa sasa wameishaambiwa wahame kwa kuwa mwenye nyumba anataka kuibomoa kwa ajili ya ujenzi.
Kwa maoni,ushauri,msaada,tuwasiliane kwa namba 0787239480,0759891849,0713290944MTOT
Mnanka katikati mara baada ya kupokewa darasa la kidato cha kwanza Kambarage sekondari mkondo D.
Mnanka akiwa na Julius Anthony Miongoni mwa watu wanaofuatilia na kusaidia matatizo ya familia hiyo wakisubiri maelekezo ya Mwalimu
Mwalimu wa Taaluma Kambarage Sekondari Peter akimpokea Mnanka na kuahidi kuwa walimu watamsaidia ili aweze kufikia malengo yake.
Mnanka anaanza kuona nuru mbele yake baada ya kuripoti shuleni kwa ajili ya kuanza masomo ikiwa ni Zaidi ya mwezi mmoja toka wamefungua shule kutokana na madhira aliyokuwa nayo.
Thursday, March 2, 2017
Home »
» MTOTO ALIYEGEUKA MLEZI WA FAMILIA AANZA MASOMO
0 comments:
Post a Comment