Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu akikata utepe kama ishara ya kupokea mradi wa maji Mtiririko katika kijiji cha Iharara uliojengwa na Kampuni ya Singita Grumeti Fund kwa ushirikiano na Shule ya Sekondari ya Issenye na wananchi,kulia kwake ni Mkurugenzi wa Singita Grumeti Fund Steven Cuniliffe.
Mradi huo utakaonufaisha wakazi zaidi ya 3500,mifugo zaidi ya 2000 umegharimu zaidi ya sh 96 milioni ,Kampuni ya Singita Grumeti Fund ikiwa imechangia zaidi ya sh 82 milioni,sekondari sh 15 mil na wananchi zaidi ya sh 2.9 mil,utapunguza ukubwa wa tatizo la wananchi wa eneo hilo na wanafunzi waliokuwa wanaacha masomo kwa ajiili ya kutafuta maji.
Picha ya pamoja baada yauzinduzi,kutoka kushoto ni afisa maendeleo ya jamii kampuni ya Singita Grumeti Fund Frida Molel,Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Iharara Goroban Mahega,Dc Nurdin Babu ,afisa mtendaji wa kijiji John Wangembe,afisa mtendaji wa kata ya Nagusi Molel na Mkurugenzi wa Singita Grumeti Fund Steven
Picha ya pamoja na wanafunzi wa Issenye sekondari katika eneo la matenki yanayopokea maji kutoka kwenye tenki kubwa kwa ajili ya matumizi ya shule.
Mkuu wa wilaya akifungulia bomba kuhakikisha maji yanayotoka kwenye chanzo cha maji mtiririko kwa kutumia umeme wa mionzi ya jua.
Afisa maendeleo ya jamii kampuni ya Singita Grumeti Fund Frida Mollel akitoa taarifa ya mradi.
Pandeni miti kote huko Dk akitoa maelekezo
Makamu Mkuu wa shule ya Issenye Ezekiel Onderi akitoa maelezo jinsi mradi utakavyowapunguzia wanafunzi na walimu umbali wa kutafuta maji.
Mwenyekiti wa serikali ya Kijiji cha Iharara Goroban Mahega akishukuru kwa kupata mradi wa maji safi na salama kwenye kijiji chake na taasisi ya shule.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Serengeti William Makunja akihimiza wananchi kushikamana na wawekezaji ili waweze kutatua changamoto zinazowakabili.
Dc anasaidni makabidhiano ya mradi
Makabidhiano yamekamilika wanapongezana.
Lango la kuingia katika chanzo kikuu cha maji eneo la mashambani linafunguliwa rasmi
Tunzeni miundo mbinu atakayehujumu atashughulikiwa kwa mjibu wa sheria.
Tuesday, March 28, 2017
Home »
» SINGITA GRUMETI FUND YAKABIDHI MRADI WA MAJI MTIRIRIKO
0 comments:
Post a Comment